Saturday, December 24, 2011

MAISHA YA WAATHIRIKA WA MAFURIKO KATIKA KAMBI YA MCHIKICHINI DAR

Mmoja wa watoto walioathirika kwa mafuriko eneo la Jangwani, akiwa amebeba baadhi ya vyombo vilivyonusurika kusombwa na mafuriko, akitoka navyo kwenye nyumba yao kwenda kwenye Kambi ya muda iliyopo Shule ya Msingi ya Mchikichini, Ilala, Dar es Salaam
Akina mama waathirika wakifua nguo zilizookolewa baada ya mafuriko, eneo la Jangwani, Dar es Salaam
Magari ya huduma ya kwanza ya JWTZ yakiwa karibu na Kambi ya waathirika ya Mchikichini
Waathirika wakiwa wamebeba moja ya tendegu la kitanda lililookolewa
Mzee aliyeathirika kwa mafuriko akipita kwenye tundu la ukuta akiwa na ndoo yenye nguo kwenda kuanika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Mchikichini ambapo imewekwa kambi ya waathirika.
Mama Hamadi ambaye ni mmoja wa waathirika akielezea insi alivyopata athari katika mafuriko eneo la Jangwani.

Baadhi ya waathirika wa mafuriko, wakijiandikisha kwa Ofisa wa Ustawi wa Jamii juzi katika kambi ya waathirika iliyopo Shule ya Msingi Mchikichini, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment