Thursday, December 29, 2011

Mutabuzi wa ITV ashinda tuzo ya AJAAT

 Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI(TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho(kushoto ) akitoa cheti na cheki ya shilingi laki saba kwa mwandishi wa habari wa ITV na Redio One Renatus Mutabuzi juzi jijini Dar es salaam wakati wa tafrija fupi ya utoaji wa zawadi na vyeti kwa washindi wa shindano la waandishi wa habari kuhusu upatikanaji wa huduma muhimu za UKIMWI kwa makundi ya watu wenye fursa chache.Tuzo hizo iliandaliwa na Chama cha Waandishi wa habari za Ukimwi Tanzania(AJAAT)
Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI(TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho(kushoto ) akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam wakati wa tafrija fupi ya utoaji wa zawadi na vyeti kwa washindi wa shindano la waandishi wa habari kuhusu upatikanaji wa huduma muhimu za UKIMWI kwa makundi ya watu wenye fursa chache. Katikati ni  Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari za UKIMWI nchini (AJAAT) bw .Simon.

No comments:

Post a Comment