Waziri Magufuli akitoa salamu za mwisho
Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mbunge wa
Jimbo la Chato leo ameshiriki kuuaga mwili wa Marehemu Constantine Jaha
Misungwi ambaye ni muasisi wa Chama cha Mapinduzi wilayani Chato.
Marehemu
Misungwi alizaliwa tarehe 01 Julai mwaka 1925 ambapo katika muda mwingi
wa uhai wake alikuwa akijihusisha sana na shughuli za kisiasa. Marehemu
Misungwi ndiye mwanzilishi wa mji wa Chato na katika nyakati tofauti
aliwahi kushika nafasi mbali mbali ikiwamo ya Uenyekiti wa Chama cha
Mapinduzi katika mji wa Chato, Udiwani na pia Uenyekiti wa Chamba Cha
Mapinduzi katika Jimbo la Biharamulo Mashariki.
Marehemu
mzee Misungwu ndiye aliyemshawishi Mheshimiwa Magufuli kujiunga na
siasa mnamo mwaka 1990 na baadaye kumchukulia tena fomu za kugombea
Ubunge wa Jimbo la Biharamulo Mashariki mwaka 1995 na kushinda kwa mara
ya kwanza.
Mmoja
ya watoto wa marehemu, Bwana Kaloli ameelezea kuwa baba yake
alilazimika kuletwa Dar es Salaam kutokea Chato kwa ajili ya matibabu ya
kansa na alilazwa kwa wiki mbili katika Hospitali ya Tumaini kabla ya
kuruhusiwa kutoka mnamo tarehe 20 Aprili 2012 lakini hata hivyo mauti
yakamfika siku mbili baadaye akiwa nyumbani kwa mwanaye huyo.Mwili wa Marehemu Mzee Misungwi umesafirishwa leo kuelekea Chato kwa mazishi
No comments:
Post a Comment