Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za
Mashirika ya Umma, Mh Zitto Kabwe amelitaarifu Bunge kuwa mchakato
unaandaliwa kukusanya saini za wabunge 70 ili kuweza kupeleka hoja ya
kulitaka Bunge kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.
Zitto amesema zoezi zima la saini hizo
linaanza kesho asubuhi Mlangoni ili kabla ya Jumatatu liwe limekamilika
ili kuweza kuwasilisha hoja hiyo ili Wabunge na Bunge limshinikize
Waziri mkuu kujiuzulu au vinginevyo mawaziri wote waliotajwa kuhusika na
ubadhirifu wa fedha za umma katika ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG) wawe wamejiuzulu badala yake.
Hii imetokea jioni hii Bungeni Dodoma
ambapo wabunge wengi bila kujali itikadi za vyama vyao wameonekana
kukerwa na utendaji mbovu wa mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete.
No comments:
Post a Comment