Basi
aina ya Coaster waliokuwa wakisafiria abiria zaidi ya 40, lenye nambari
za usajili T 374 AVR, likiwa limepinduka baada ya kugongwa kwa nyuma na
basi jingine la kampuni ya El Saedy lenye nambari T 499 AVG. Tukio
lililotokea Aprili 23 mwaka huu saa moja asubuhi eneo la Imezu na Inyala
Wilaya ya Mbeya Vijijini.
Basi la kampuni ya El Saedy lenye nambari T 499 AVG lililohusika katika ajali, baada ya kuligonga kwa nyuma basi aina ya Coaster enye nambari za usajili T 374 AVR ambapo zaidi ya abiria 40 kunusurika kifo. Tukio lililotokea Aprili 23 mwaka huu saa moja asubuhi eneo la Imezu na Inyala Wilaya ya Mbeya Vijijini.
---
Picha na Habari: Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Abiria
zaidi ya 40 wamenusurika kifo baada ya basi waliokuwa wakisafiri aina
ya Coaster, lenye nambari za usajili T 374 AVR, kupinduka lilipogongwa
kwa nyuma na basi jingine la kampuni ya El Saedy lenye nambari T 499
AVG.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa basi la El Saedy likiwa katika hali ya
mwendokasi liliharibika mfumo wa breki kutoka eneo la Mlima Nyoka na
kuligonga basi hilo dogo kwa nyuma katika mteremko wa Shule ya Sekondari
Imezu, hali iliyopelekea basi hilo dogo kupinduka.
Baada
ya Coaster kupinduka basi la El Saedy likiwa bado katika mwendokasi
liliendelea na safari, kabla ya dereva kufanikiwa kulichepusha kabla
halijavuka reli ya TAZARA katika Kijiji cha Inyala Wilaya ya Mbeya
Vijijini.
Aidha
baadhi ya abiria katika basi hilo dogo walikuwemo wanafunzi 28, wa kike
na kiume wakielekea shuleni majira ya saa moja asubuhi, Aprili 23 mwaka
huu katika Shule ya Sekondari Imezu.
Mara
baada ya ajali hiyo kutokea baadhi ya abiria walikuwemo katika basi
hilo dogo walikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa Jijini Mbeya, ambapo
kati yao wamelazwa ili kufanyiwa uchunguzi na wengine wakiruhusiwa
kurudi nyumbani.
Kaimu
Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Mbeya Barakiel
Masaki,hakupatikana kuelezea ajali hiyo ingawa dereva wa basi la El
Saedy anashikiliwa na Polisi kwa mahojiano.
Picha na Habari: MbeyaYetu Blog.
No comments:
Post a Comment