Sunday, August 21, 2011

PRECISION AIR YAANZA SAFARI HAHAY - COMORO

Abiria wa kwanza kusafiri na Precision Air kutoka Komoro walionekana kufurahia huduma hiyo ya ndege.  Jumla ya abiria walikuwa 110, ndege iliyofanya safari hiyo ni aina ya Boeing 737-300 yenye uwezo wa kubeba abiria 116.
Ndege aina ya Boeing 737-300 ilivyotua kwa mara ya kwanza uwanja wa ndege wa kimataifa wa Prince Ibrahim.
Mkurugenzi Mkuu na Meneja Mwendeshaji wa Precision Air Bw. Alfonse (kulia) akikaribishwa na mwenyeji wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi nchini Komoro Bw. Abdulahi Mwinyi mara baada ya kuwasili na safari ya kwanza ya shirka ya ndege hiyo kutokea uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere-Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu na Meneja Mwendeshaji wa Precision Air Bw. Alfonse Kioko akiteta na Mwenyekiti wa Galaxy General Sales Agents, Bw. Nassor Ali. Kampuni ya Galaxy ni wakala rasmi wa Precision Air nchini Comoro.
. Mkurugenzi Mkuu na Meneja Mwendeshaji wa Precision Air Bw. Alfonse Kioko akisindikizwa kwenda kupanda ndege na wenyeji wake baada ya uzinduzi mfupi uliofanyika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Prince Ibrahim, Hahaya-Komoro. 
Afisa Mawasiliano wa Precision Air, Bw. Amani Nkurlu akiwa na wana anga wa shirika la ndege hilo walioshiriki kufanikisha safari ya kwanza ya kwenda na kurudi Hahaya-Komoro kutokea Dar es Salaam jumatano iliyopita.

No comments:

Post a Comment