Monday, August 29, 2011

NAIBU SPIKA MH. JOB NDUGAI AONGELEA UVUMI AMBAO UMEZAGAA KUHUSU KUTOFAUTIANA NA SPIKA


Mh. Job Ndugai (Naibu Spika)
     Taarifa ambayo imeibuka kuhusu Spika na Naibu Spika kutofautiana kuhusu maamuzi ya kuunda Kamati maalum ya kumchunguza Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Ndg. David Jairo si ya kweli.
     Mh. Job Ndugai ameyaongea haya katika kipindi cha Jahazi cha Clouds FM cha leo na amekana huo ni uvumi tu wa watu ambao wasiolitakia mema taifa letu na wasioutakia mema ushirikiano wao mzuri ambao wanao yeye na Mh. Spika Anna Makinda, na vile vile Mh. Ndugai alilielezea pia uvumi ambao watu wameuzusha kuhusu yeye kuonekana ana nguvu zaidi ya Spika Anna Makinda; Mh. Ndugai amekana hilo na kusema ni maneno tu yale yale! ambayo watu wasioutakia mema ushirikiano wao na kusema kwamba Mh. Spika Anna Makinda anamuamini sana na anamtuma katika shughuli nyingi tu ambazo ni muhimu lakini anaenda yeye Mh. Job Ndugai.     Clouds Fm walimuuliza maswali mawili matatu naye akayaongelea kwa ufasaha na kutaka wananchi waelewe hivyo anavyosema yeye, kuliko kusikiliza watu ambao wanazusha tu mambo ambayo sio mazuri

No comments:

Post a Comment