Wednesday, August 24, 2011

ADEBAYOR AJIUNGA NA SPURS KWA MKOPO



Tottenham wamefanikiwa kukamilisha usajili wa mkopo kutoka Manchester City na kuwapiku Inter Milan ambao walianza harakati za siri za kumnyakua mshambuliaji huyo.
Adebayor hatoruhusiwa kuichezea Spurs dhidi ya City weekend hii.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal, atafanyiwa vipimo jijini London Jumatano baada ya Tottenham kukubali kuchangia kwa kiasi kikubwa mshahara wa 170,000 kwa wiki.
Dili hilo lilichelewa kutokana na mshambuliaji huyo kukataa kupunguza mshahara wake baada ya kukatwa katika kikosi cha kwanza na kocha Roberto Mancini.
Wakati huo huo Inter Milan walitumia masaa 11 kufanikishampango wa kumchukua Adebayor, lakini kipindi hicho hicho Tottenham walikuwa katika hatua za mwisho straiker huyo aliyekuwa kwa mkopo Real Madrid msimu uliopita.

No comments:

Post a Comment