Monday, August 22, 2011

TWANGA PEPETA KUSHAMBULIA T.T.C CLUB SIKU YA EID PILI

Bendi maarufu nchini African Stars `Twanga Pepeta, itatumbuiza katika onyesho maalum ijulikanalo kama ‘Konyagi Iddi Pili Show’ ambalo limepamgwa kufanyika kwenye ukumbi wa TCC Club, Chang’ombe, Temeke siku ya Iddi Pili.

Mratibu wa onyesho hilo, Joseph Kapinga, amesema hilo la pekee la aina yake limeandaliwa na Bob Entertainment chini ya udhaminbi wa kinywaji cha Konyagi.

Kapinga alisema burudani hiyo ni maalum kwa ajili ya kusindiza sherehe ya Iddi Pili.

Naye mkurugenzi wa bendi hiyo, Asha Baraka, amesema kuwa onyesho hilo litatumika kutangaza albamu yao mpya inayotarajiwa kutambulishwa rasmi baadaye mwaka huu.

Nyimbo zilizomo kwenye albamu mpya ya Twanga Pepeta ni pamoja na Kauli, Kiapo cha Mapenzi, Umenivika Umasikini, Mtoto wa Mwisho, Dunia Daraja na Penzi la Shemeji.

Kapinga alisema kuwa onyesho la TCC pia litatumika kumtambulisha Kimwana wa Twanga Pepeta 2011 Mary Khamis ambaye amejiunga na bendi hiyo kuchukua nafasi ya mnenguaji Aisha Madinda aliyetimkia katika Bendi ya Extra Bongo.

Mcheza show huyo pamoja na wanamuziki wengine wa bendi hiyo watataonesha ustadi wao katika kusakata mitindo ya Twanga Pepeta.

Twanga Pepeta ina wanenguaji wa kike tisa na wa kiume wanne, ambao ni Abdillahi Zungu, Kassim Mohammed au Super K, Bakari Kisongo au Mandela na Said Mtanga hao ni safu ya unenguaji wa kiume.
Kwanza upande wa wanawake ni pamoja na Fasha Sunday, Beatrice Mwangosi au Baby Tall, Asha said au Asha Sharapova, Regina Filbert, Grace Kaswaga, Vicky Pandapanda, Lillian Tungaraza au Internet, Sabrina Mathew na Maria Soloma.

Pia Twanga Pepeta litatumbuiza siku ya Iddi Mosi Kwenye Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni na Iddi Tatu katika ukumbi wa Habours Club, Kurasini

No comments:

Post a Comment