Monday, August 29, 2011

Mpigie kura yako Nelly Kamwelu


Miss Universe Tanzania 2011, Nelly Kamwelu, akiwa amepozi wakati wa zoezi la upigwaji picha muda mfupi baada ya kuwasili katika mji wa São Paulo, Brazil. 

Kamwelu atakuwa katika mji huo kwa wiki 3 akishiriki katika matukio mbalimbali na kujiandaa na shindano la 2011 MISS  UNIVERSE linalotaraji kufanyika September 12 kuanzia majira ya saa  9:00 p.m. 

Shindano hili litatangazwa moja kwa moja na kituo cha Televisheni cha NBC kutoka katika ukumbi wa  Credicard Hall uliopo mjini São Paulo, Brazil. 

Mtanzania popote pale ulipo duniani unaombwa kumpigia kura mshiriki huyu na mwakilishi wa taifa ili aweze kufuzu hatua ya nusufainali.


Kumpigia Nelly Kamwelu kura yako ingiahapa chini:-

No comments:

Post a Comment