Thursday, August 18, 2011

TRACY SOSPETER AWA MREMBO WA PILI KUTINGA NUSU FAINALI YA VODACOM MISS TANZANIA BAADA YA KUTWAA TAJI LA MISS PHOTOGENIC 2011

Mshindi wa taji la Miss Photogenic 2011, Tracy Sospeter kutoka Mkoa wa Shinyanga na Kanda ya Ziwa, akiwa katika poazi baada ya kutajwa kuwa ndie mshindi katika shindano hilo dogo katika shindano la Vodacom Miss Tanznia 2011 na kufanikiwa kuwa mrembo wa pili kuingia katika hatua ya 15 bora ya shindano hilo. Mshindi huyo alitangazwa akiwa mjini Arusha leo.
 Baadhi ya washiriki wa Vodacom Miss Tanzania 2011, wakisoma jarida la Vodacom katioka ofisi za Arusha hii leo.
Mkurugenzi wa Lino International Agency, waandaji wa Shindano la Vodacom Miss Tanzania, Hasim Lundenga akitangaza matokeo ya shindi wa shindano la Vodacom Miss Photogenic 2011. Kulia ni Mkurugenzi wa Vodacom Kanda ya Kaskazini, Nguvu Kamando.
 Watumishi wa Vodacom Arusha wakiwa katika mkutano huo.
Warembo Vodacom Miss Tanzania 2011, waliofanikiwa kuingia tano boira ya shindano la Miss Photogenic 2011 kutoka kulia , Trecy Sospeter,Jeniffer Kakolaki, Chiaru Masonobo, Christine William na Glory Lori wakipozi kwa picha ya pamoja baada ya kutajwa kufanikiwa kuingia katika hatua hiyo jana mjini Arusha
Vodacom Miss Photogenic 2011, akipozi mbele ya camera. Tracy Sospeter amekuwa mrembo wa pili kutinga nusu fainali ya Vodacom Miss Tanzania.

No comments:

Post a Comment