Sunday, August 21, 2011

AIRTEL WATOA MSAADA WA VITABU MOROGORO

 

Meneja Mauzo  Kanda ya Pwani wa kampuni ya simu ya Airtel, Aluta Kweka (kushoto), akikabidhi sehemu ya msaada wa vitabu kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro, Alfred Shayo vilivyotolewa na kampuni hiyo kwa Shule za Sekondari za SUA, Mwembesengo, Mji Mpya na Mgulasi Mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Sekondari ya SUA, Khalfan Millongo, Meneja Huduma za Jamii wa Airtel Tunu Kavishe na Diwani wa Kata ya Mbuyuni, Samuel Msuya. Vitabu hivyo vina thamani ya shs milioni 4.
Meneja Huduma za Jamii wa Airtel Tanzania, Tunu Kavishe (wa tatu kushoto) akikabidhi sehemu ya msaada wa vitabu kwa mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari SUA, Rogers Shempemba vilivyotolewa na kampuni hiyo kwa Shule za Sekondari za SUA, Mwembesengo, Mji Mpya na Mgulasi Mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja Mauzo wa Airtel Kanda ya Pwani, Aluta Kweka na Mkuu wa Sekondari ya SUA, Khalfan Millongo.
Meneja Mauzo  Kanda ya Pwani wa kampuni ya simu ya Airtel, Aluta Kweka (kushoto), akikabidhi sehemu ya msaada wa vitabu kwa mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari SUA, Happiness Makundi vilivyotolewa na kampuni hiyo kwa Shule za Sekondari za SUA, Mwembesengo, Mji Mpya na Mgulasi Mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki. Wa pili kushoto ni Meneja Huduma za Jamii wa Airtel, Tunu Kavishe na kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro, Alfred Shayo. Vitabu hivyo vina thamani ya shs milioni 4.

No comments:

Post a Comment