Tuesday, August 16, 2011

WAKUFUNZI WA SENSA YA MAJARIBIO WAPATA MAFUNZO

Baadhi ya wakufunzi wa Sensa  ya majaribio ambayo inatarajia kufanyika  kuanza Septemba 4 mwaka huu wakiwa katika mafunzo ya wiki moja jana mjini Morogogoro . Wakufunzi hao wanatarajiwa kusambazwa katika maeneo mbalimbali nchini tayari nao kwa ajili ya kuendesha mafunzo kwa watu watakaohusika na sensa.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu  Dr. Albina Chuwa (kushoto) akijadiliana jambo na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Said Mwambungu  wakati wa ufunguaji wa mafunzo ya wiki moja ya wakufunzi wa Sensa ya majaribio yalioanza jana mjini Morogoro ambayo yamewashirikisha wadau mbalimbali. Wakufunzi hao watasambazwa sehemu mbalimbali kwa ajili ya kuendesha mafunzo kwa watu watakaohusika na Sensa ya majaribio inayoanza Septemba 4 mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Kanali Mstaafu Issa Machibya(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wakufunzi wa Sensa ya majaribio ambao wanashiriki mafunzo ya wiki moja ya wakufunzi wa Sensa  ya majaribio itakayofanyika kuanzia  kuanza Septemba 4 mwaka huu nchini kote. Wakufunzi  hao wanatarajiwa kusambazwa sehemu  mbalimbali ili kutoa mafunzo kwa watu watakaoshiriki kuendesha Sensa ya majaribio .

No comments:

Post a Comment