Thursday, October 20, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AHUDHURIA SHEREHE ZA KUMBUKUMBU YA KIFO CHA SAMORA MACHEL-MAPUTO


 Makamu wa Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akiteta jmabo na Rais wa Afrika ya Kusini, Jacob Zuma, wakati walipokutana na katika viwanja vya Mozambiq Heroes Square, kwenye sherehe za maadhimisho ya Kumbukumbu ya kifo cha mwasisi wa nchi hiyo, Samora Machel, zilizofanyika jana Oktoba 19, mjini Maputo. Kulia kwa Makamu ni Mama Zakhia Bilal na (katikati) ni Rais wa Afrika ya Kusini, Jacob Zuma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na aliyekuwa mke wa Rais wa zamani wa Mozambiq, Mama Graca Machel, wakati walipokutana na katika viwanja vya Mozambiq Heroes Square, kwenye sherehe za maadhimisho ya Kumbukumbu ya kifo cha mwasisi wa nchi hiyo, Samora Machel, zilizofanyika ljana Oktoba 19, mjini Maputo. Kulia kwa Makamu ni Mama Zakhia Bilal na (katikati) ni Rais wa Afrika ya Kusini, Jacob Zuma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,mkewe Mama Zakhia Bilal na Mama Maria Nyerere,wakiwa pamoja na baadhi ya Marais wan chi za Afrika wakati walipohudhulia katika sherehe za maadhimisho ya Kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Mwasisi na Rais wa Mozambiq, Samora Machel, zilizofanyika jana Oktoba 19 mjini Maputo Msumbiji.
Mama Maria Nyerere akiweka Shada la Maua ndani chumba maalum mahala lilipo kaburi la mwasisi wan chi ya Mozambiq, wakati wa maadhimisho ya sherehe za kumbukumbu ya kifo cha mwasisi huyo zilizofanyika mjini Maputo Msumbiji jana
Kingunge Ngombale Mwilu, akijumuika na wananchi wa nchini Mozambiq, kuelekea kuweka mashada ya maua katika kaburi la Mwasisi wa nchini hiyo, wakati wa sherehe za maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa rais wan chi hiyo, Samora Machel, zilizofanyika jana.
Askari wakimuongoza Rais wa Mozambiq, Armando Guebuza, kuelekea kuweka Shada la maua katika Kaburi la Mwasisi wan chi hiyo, ambaye pia aliwahi kuwa Rais wa nchini hiyo, Samora Machel, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Mwasisi na Rais wa Mozambiq, Samora Machel, zilizofanyika jana.

No comments:

Post a Comment