Thursday, October 6, 2011

MISS TOURISM MARA 2011/2012- WAREMBO WATAMBIANA USHINDI

Doreen Charles- 20
Anauhakika atashinda, Miss Tourism 2011/2012 Na atakua tayari kutangaza Vivutio vya Mkoa wa Mara Hasa Makumbusho ya Mwalimu Nyerere yaliyopo Butiama. Kwani wengi wamezoea Vivutio vya Ziwa Victoria na Mbuga ya Wanyama, Serengeti.
Ugenia Masatu- 21
Amejiandaa vizuri na mashindano na matarajio yake ni Ushindi. Endapo atabahatika kuwa Miss Tourism Mara. Atashirikiana na Taasisi mbalimbali kuutangaza utalii mkoani Mara na vilevile atakua tayari kuwaelezea wakazi wa mara faida za utalii na kuwahimiza kutembelea vivuto vinavyopatikana Mkoani Mara.
Gaudensia Joseph- 21
Amejiandaa vizuri na uhakika wa kushinda anao kwa sababu anajiamini. Iwapo atashinda taji la Miss Tourism Mara, atakua balozi mzuri katika mkoa wa Mara na kuweza kuhamasisha jamii kuondoa mila na desturi ambazo hazileti maendeleo katika mkoa wa Mara.
Suzana
Anajiamini atashinda, na yeye ndiye mshindi wa taji la Miss Tourism Mara 2011/2012. Matarajio yake baada ya kushinda taji ni kutangaza utalii wa ndani kwa nguvu zote.
Winfreda David- 21
Mategemeo yake ni kuwa mshindi, kwa sababu anajiamini na kujitambua yeye ni mrembo wa utalii. Iwapo atashinda taji la Miss Tourism Mara, ni kuwasaidia watoto yatima na watoto walio katika mazingira hatarishi.
Teddy James- 20
Anataraji kuwa mshindi kwa sababu ana vigezo vinavyostahili. Iwapo atashinda taji la Miss Tourism Mara 2011/2012 anataraji kutoa elimu kuhusu madawa ya Kulevya.
Veronica Fredrick- 18
Matarajio yake ni ushindi kwa sababu anajiamini kwa kile anachokifanya na amejiandaa kikamilifu. iwapo atashinda taji la Miss Tourism atakua tayari kuwasadia wajane, watoto yatima na waathirika wa Ukimwi.
Veronica Josephat- 19
Anataraji ushindi, kwa sababu anajiamini na anamvuto unaokubalika. Iwapo atashinda taji la Miss Tourim Mara 2011/2012 atazuia mila potofu za ukeketaji kwa wanawake.
Ramla Yunus- 21
Anataraji Kunyakua taji la Miss Tourism Mara 2011/2012 kwa sababu ana vigezo vyote kwa sababu amewasoma wenzake na kukuta wana mapungufu, kutokana na urembo wake na ufahamu wa mambo ya utalii na Utamaduni wa Mkoa wa Mara. Iwapo atashinda anataraji kuielimisha jamii kuhusu mila potufu ya kuwafanyia wasichana tohara na kuutangaza utalii wa ndani wa mkoa wa Mara.
Jasmine Salum- 20
Anasema tayari yeye ni mshindi wa Taji la Miss Tourism Mara 2011/2012 na atakua tayari kulinyakua taji la kanda ya ziwa na kunyakua taji la taifa. Anajiamini na anamvuto unaokubalika.
Anataraji kusaidia watoto yatima, waathirika wa ukimwi na watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi

No comments:

Post a Comment