Wednesday, October 12, 2011

LULU NI MFUASI WA DINI YA MASHETANI..?

  Msanii wa filamu Elizabeth Michael"lulu" ametupia picha kadhaa facebook yake zenye uashirio wa alama za dini ya waabudio shetani kama anavyoonekana pichani hapo juu.
   Alama hiyo inamaanisha kichwa cha mnyama chenye pembe mbili ambapo humaanisha ufalme wa giza "lusifa" yaani ufalme wa shetani huko kuzimu.
    Alama nyingi za dini ya waabudio shetani ziko kwenye tatuu na watu wengi hujichora tu bila kujua maana halisi ya tatuu husika,dini hii imekumba mastaa wengi,wasanii,wanasiasa na wanamichezo duniani kwani huwavutia kwa kuwapa uvuvio wakuwa mastaa wa kidunia na fedha nyingi wakiwamo wale wanaongoza kwa fedha nyingi duniani.
   Nilifanya mahijiano ya simu na Lulu kuhusu matumizi ya alama hizi katika picha zake alishtuka na kudai yeye hajui chochote aliona ni moja ya pozi tu la picha lakini alijibu kwa hofu kana kwamba mtu kamkurupua kwa kitisho cha gafla,kumbe unaweza kumwabudu/kumtukuza shetani bila kujua ni vema ukawa makini kuiga mambo usiyoyajua.

No comments:

Post a Comment