Monday, October 3, 2011

TAMASHA LA TUSKER ALL STAR LASHIKA NAIROBI

Mmoja wa madada wakali katika miondoko ya hipo hop nchini Marekani,Eve E akiwaachia mistari wakazi wa Nairobi,ambao wengi wao walikuwa wakivutiwa nae kwa namna ambavyo alikuwa akionesha kukomaa kwake
kwenye anga ya muziki wa hip hop.
Shaggy ni mmoja wa wanamuziki ambao kiukweli awapo jukwaani hana masikhara kabisa na uwanja wake,kila wakati hupenda kuhakikisha watu wanashangweka tu,na ndivyo ilivyokuwa kwenye shoo yake usiku wa leo,kila wakati alikuwa akiwaimbisha mashabiki nao bila hiyana walikwenda nae sambamba,hali iliyomfurahisha zaidi.
Pamoja na kuwepo kwa hali ya mvua mvua,lakini maelfu ya watu waliokuwa kwenye viwanja vya carnivo kujiachia ndani ya tamasha la Tusker All Stars 2011,hawakutaka kubanduka kabisa,badala yake walikuwa wakijifunika na viti ili wasikose uhondo uliokuwa ukiendelea kutolewa jukwaani.

No comments:

Post a Comment