Thursday, October 6, 2011

Mgunduzi wa Apple, iPhone, iPad, iPod, iMac na iTunes, amefariki


Steve Jobs  mgunduzi wa Kompyuta na Bidhaa maarufu duniani zenye uwezo wahali ya juu wakufanya kazi za Apple, iPhone, iPad, iPod, iMac na iTunes,  amefariki, Kampuni yake uya Apple imesema. Jobs amefariki  akiwa na umri wa miaka 56.
 "Tunamajonzi makubwa san asana kutangaza kuwa Steve Jobs amefariki hii leo,” ailisomeka taarifa  iliyotolewa na Bodi ya wakurugenzi wa Apple’s. "Uwezo mkubwa wa Steve katika  kufikiri, kujituma vilikua njia kuu ya ugunduzi  wake ambao umechangia kuendeleza maisha yetu sote. Dunia imekua mahali pazuri kwasababu ya Steve. Mapenzi yake makubwa yalikuwa ni kwa mkewe Laurene, na familia yake. Mioyo yetu ilikuwa kwako na wote waliobarikia kupata zawadi hiyo ya kipekee.”
Ukurasa wa tovuti ya  Apple's leo ulijaa picha kubwa ya Jobs ukiwa na maandishi "Steve Jobs 1955-2011."
Ukibofya katika picha hiyo unakutana na maelezo ya ziada kuwa : "Apple wamepotea kichwa chenye muono na  akili nyingi ya ubunifu, dunia pia imempoteza mtu muhimu sana.
Job  aliyeanza ugunduzi wa Kompyuta za Apple mwaka 1976 akiwa na rafiki yake wa utotoni Steve Wozniak, na waligundua kompyuta binafsi ya kwanza duniani aina ya  Apple II.
Mwaka  2004, alianza kuugua saratani kongosho iliyopelekea mwaka  2009 alibadilishwa Ini lake  . Aidha baada ya kuendelea kuugua 24 Agosti 2011 , Job alitangaza kujiuzulu wadhifa wake wa Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) katika kampuni hiyo.
“ Siku zote nilikuwa nikisema, kama kuna wakati utafika wa mimi kushindwa kutekeleza majukumu yangu kama Mkurugenzi Mtendaji wa Apple, nitakuwa wa kwanza kuwajuliasha,” Job aliandika katika barua yake ya kujiuzulu. “Kwa bahatimbaya siku hiyo imefika.”
Akiwani mmoja wa ma- CEO maarufu diniani, Job hakuwa mtu wa kupenda kufanya mahojiano na waandishi na kuzungumzia maisha yake binafsi  na alimkataza mkewe na watoto wake pia kufanya hivyo katika jamii.
"Hakuwahi kuwa mtu wa kuzungumza na vyombo vya habari,” alisema mmoja wa  wachambuzi wa masuala ya viwanda  Tim Bajarin, baada ya kujiuzulu kwa Job.   "Alikuwa akiruhusu mahojiano wakati tu wa kuzindua bidhaa mpya, tena iliyo na manufaa kwa Apple, lakini kamwe sijawahi muona au kusikia akizungumzia maishayake binafsi.

No comments:

Post a Comment