Mkurugenzi wa Airtel Tanzania, Sam Elangallo.
October 16 2011, Airtel Tanzania imetangaza kuongeza siku tatu zaidi kwa wateja wake wote wanaotumia huduma ya blackberry kutokana na tatizo la mtandao lililotokea hivi karibuni na kuathiri mtandao wa internet kwa blackberry ulimwengu mzima.
Tatizo lililoathiri mtandao tayari limesharekebishwa na watoa huduma hiyo kwenye mtandao wa blackberry ambapo imegundulika tatizo la kukosekana huduma hiyo lilisababishwa na itilafu iliyoathiri mfumo wa mtandao wa kutuma ujumbe na peruzi kwa njia ya mtandao ulimwenguni kote lililodumu kwa siku tatu mfululizo. Tatizo hili lilianzia Ulaya na kuzikumba pia nchi za Mashariki ya kati, Afrika, na India kisha kusambaa kaskazini mwa Amerika.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Airtel Tanzania Bw Sam Elangallor amesema “Tunasikitishwa sana na tatizo lilowakumba wateja wetu wanaotumia huduma ya blackberry hivi karibuni hivyo leo naomba niwajulishe wateja wetu wote yaani wa malipo kabla na baada tunawaongezea siku 3 kuendelea kutumia huduma hiyo bila malipo mara baada ya kifurushi cha mwezi octoba kuisha. Tutaendelea pia kuwajulisha wateja wetu wote kuhusu kuongezewa siku hizi 3 kupitia njia ya sms ili kila mmoja afahamu kuwa fidia imefanyika kwa tatizo alilopata.
Sam Elangallor “wateja wetu wa malipo baada, ambao hulipa Ankara zao kwetu kila mwisho wa mwezi pia wataongezewa siku tatu katika huduma ya blackberry kwa mwezi huu wa octoba. Ongezeko la kutumia huduma ya blackberry bila malipo kwa siku tatu kwao litaonekana katika taarifa zao za malipo zinazotolewa kwao kwa mwezi October.
Airtel inatambua kuwa tatizo la kukosekana kwa mtandao kwa wateja wake wanaotumia huduma za blackberry halikusababishwa na mitambo ya Airtel bali ni itilafu iliyotokea kwenye mtandao ulimwenguni kote hivyo kuona kunaumuhimu wa kuwarudishia wateja wake huduma bure kwa siku 3 ambazo hawakupata huduma hiyo
No comments:
Post a Comment