Friday, October 7, 2011

MR.FLAVA KUTUMBUIZA FAINALI ZA BSS

Ile fainali ya shindano la kumsaka mkali wa kuimba la Bongo Star Search ‘Second Chance’ 2011, inatarajiwa kuchukua nafasi Oktoba 14, mwaka huu (Ijumaa), ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na mtandao huu mapema leo, mkurugenzi wa BSS, Rita Paulsen ‘Madam’ alisema kuwa fainali hiyo itatumbuizwa na msanii mkubwa kutoka nchini Nigeria, Chinedu Okoli N’Abania ‘Mr Flavour’ anayetamba na wimbo wa Ashawo.

No comments:

Post a Comment