Thursday, October 13, 2011

KAGO AREJEA MSIMBAZI, TIMU IPO KAMBINI




Straiker wa kimataifa wa Simba, Gervas Kago, amerejea jana jijini Dar es Salaam na kujiunga na kambi ya timu hiyo kujiandaa na mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya African Lyon inayotarajiwa kupigwa Oktoba 16 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga ‘Mr. Liverpool’, alisema kurejea kwa Kago ambaye alikuwa Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa ajili ya kuichezea timu ya taifa ya nchi hiyo ambayo ilikuwa ikitafuta tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika (CAN), kutaiongezea makali timu yao ili iweze kufanya vema katika mechi zake za kumaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Alisema, tayari Kago ameshajiunga na wenzake ambao wamepiga kambi Bamba Beach, Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi zilizobaki, ambapo alibainisha kuwa wachezaji wa timu hiyo waliokuwa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ nchini Morocco, ambao ni Juma Kaseja, Said Nassor ‘Cholo’, Juma Jabu na Juma Nyoso nao wameshaingia kambini.

No comments:

Post a Comment