Tuesday, October 25, 2011

UTURUKI WATOA MSAADA WA INCUBATORS 10 WAMA


Mwenyekiti wa WAMA na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimshukuru balozi wa Uturuki Nchini, Dkt Sander Gurbuz, baada ya kupokea msaada wa mashine 10 za kusaidia watoto waliozaliwa kabla ya muda wao. Mashine hizo, zenye thamani ya dola 30,000 (kama milioni 50), zimetolewa na kampuni ya madini na nishati ya Uturki iitwayo TPM ambapo Mkurugenzi Mkuu wake Bw Burak Buyuksaar (wa tatu kulia) alikuwepo kushuhudisa makabidhiano hayo. Kulia ni mke wa balozi, Mama Durhan Gurbuz.
Ubalozi wa Uturuki nchini Tanzania umetoa msaada wa incubators 10 zenye thamani ya Tsh. Mil 50/- kwa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) inayoongozwa na Mhe. Mama Salma Kikwete, Mke wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. 

Akikabidhi msaada huo Balozi wa Uturuki hapa nchini Mhe. Dr. Sander Gurbuz amesema kuwa wametoa msaada huo kwa ajili ya kusaidia moja ya programu za Taasisi ya WAMA inayolenga kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto. Pamoja na kudumisha uhusiano mzuri ambao nchi yake ya Uturuki na Tanzania umekuwa nao. 
Mhe. Balozi aliambatana na Mke Wake Mama Durhan Gurbuz na Mkurugenzi Mkuu wa TPM Mining and Energy Co. Limited, Bw. Burak Buyuksarac. 
Akitoa shukrani baada ya kupokea msaada huo Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mhe. Mama Salma Kikwete amesema kuwa msaada huo ni mkubwa sana na utasaidia kuokoa maisha ya watoto wachanga ambao wangeweza kufa kutokana na ukosefu wa vifaa hivi hasa maeneo ya vijijini. 
Mama Salma aliongeza kuwa pamoja mazingira ya Vijijini yanaweza yasiruhusu sana utumiaji wa vifaa hivi lakini kwa sababu siku hizi kuna umeme wa jua utasaidia matumizi ya vifaa hivi.

No comments:

Post a Comment