Wednesday, October 12, 2011

NYALANDU ATEMBELEA WAKALA WA VIPIMO NA MIZANI.

 

 Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu ( Aliechuchumaa kulia) na Meneja wa Vipimo na Mizani Mkoa wa Ilala Bw Hamisi Hamidu (kushoto) wakiangalia kipimo cha kutambua usahihi wa mafuta yanayopita katika pampu za kuuzia bidhaa hiyo. Wanaotazama ni maafisa wa Wakala wa Vipimo na Mizani na wenzao kutoka 
Wizara ya Viwanda na Biashara.
 Gari la kubeba mafuta kama lilivyokutwa likihakikiwa vipimo vyake katika karakana na Wakala wa Vipimo na Mizani.
 Aina mbali mbali za mizani zinazotumika katika kupima uzito wa bidhaa.
   Meneja wa Vipimo Mkoa wa Ilala Bw Hamisi Hamidu (kushoto) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu ( Mwenye suti katikati) katika ziara yake Jijini Dar es salaam leo. 
Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa Wakala wa Vipimo na Mizani na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu(Aliekaa katikati) mara baada ya ziara yake kuwatembelea.  
*************************************
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu, leo ametembelea taasisi ya Wakala wa Vipimo na Mizani iliyo chini ya Wiuzara yake ili kuonana na wafanyakazi na kujionea baadhi ya shughuli zao.

Naibu Waziri Nyalandu amepokelewa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala huo Bwana Deo Maneno na kupewa taarifa ya utendaji wa taasisi hiyo ambayo imeonesha mafanikio makubwa katika kulinda haki za watumiaji hasa wakulima dhidi ya vipimo batili.

Akizungumza na Wafanyakazi na Vyombo vya habari mara baada ya ziara yake, Mh Nyalandu ameitaka taasisi hiyo kuongeza juhudi katika kudhibiti vipimo ili kuhakikiksha kuwa, watumiaji wanapata bidhaa na huduma zinazolingana na thanmani ya fedha wanazotoa.

Ameahidi kuusaidia Wakala huo ili kupata sheria mpya yenye nguvu zaidi kuliko ilivyo sasa ambapo wakosaji huamriwa kulipa faini ndogo zinazowafanya kuendelea kutumia vipimo batili bila wasiwasi wowote.

“ Kazi yenu ni muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa, watu wa kada zote wanawategemea katika kupata haki.. Kuanzia wakulima mpaka wanunuzi wa bidhaa za viwandani, wote wanataka vipimo sahihi,pigeni vita kangomba na lumbesa, shirikianeni na mamlaka nyingine kutimiza wajibu huu, wajengeeni watumishi wenu mazingira bora ya kazi, mtafanikiwa kuliko ilivyo sasa”, amesema Nyalandu.

No comments:

Post a Comment