Thursday, October 13, 2011

BREAKING NEWS: VIDIC AASTAFU SOKA




Nahodha wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Serbia Nemanja Vidic ametangaza kustaafu kucheza soka la kimataifa baada ya timu yake ya Serbia kukosa nafasi ya nafasi ya kushiriki michuano ya ulaya mwakani.
Vidc ambaye alikosa penati na kupelekea timu yake kufungwa 1-0 na Slovenia jana Jumanne hivyo kuikosesha Serbia nafasi ya kucheza play offs kwa ajili ya EURO 2012.Estonia walimaliza wa pili huku Italy wakishika usukani mwa kundi C.
Vidic mwenye miaka 29 alisema: “Muda wa mabadiliko ya kizazi kipya na wachezaji wakubwa kusema kwaheri kwa jezi ya Serbia.
Pia kiungo wa Inter Milan Dejan Stankovic mwenye miaka 33 ambaye nae ametangaza kustaafu alisema: “Nimecheza mechi nyingi, nimeisaidia timu ya taifa na sasa ni muda wangu kugeukia majukumu yangu katika klabu yangu ya Inter MiLAN.

No comments:

Post a Comment