Thursday, October 27, 2011

DULAYO D- TIMING KUSHAMBULIA BAGAMOYO INTERCOLLEGES NIGHT 2011 KESHO

 Dulayo D-timing


Msanii wa muziki wa kizazi kipya Abdulrahman Kasembe a.k.a Dulayo D-Timing anatarajia kuwaongoza wasanii wengine kutoa burudani  katika usiku wa wanavyuo ujulikanao kama Bagamoyo Intercolleges Night.Pamoja na Dulayo kutakuwa na wasanii wengine wa muziki wa asili na muziki wa disko utakaoporomoshwa na dj Nature Skills.

Kwa mujibu wa bw. Kim Kimenya ,mkurugenzi wa kampuni ya Kimkev entertainment Dulayo anayetamba na nyimbo ya “twende mchumba” ataburudisha kwenye usiku huo unaotarajiwa kufanyika kesho Ijumaa tarehe 28.10.2011 kuanzia saa 2:00 usiku katika ukumbi wa Taasisi ya Sanaa na utamaduni Bagamoyo (Tasuba),ambapo tiketi za tukio hilo zinapatikana kwenye duka maarufu la nguo za kiume liitwalo Mrimi classic wear liliopo mjini Bagamoyo.

Kimenya alisema kuwa usiku huo ambao unafanyika kwa mara ya kwanza mjini Bagamoyo unatarajia kuhudhuriwa na wanavyuo wasiyopungua 1500 kutoka vyuo vya Bagamoyo na utakuwa usiku wa rangi nyeupe, ambapo watakaopendeza  kwa mavazi ya rangi nyeupe watazawadiwa fedha taslimu pamoja na kulala kwa usiku mmoja kwenye hoteli maarufu za mjini Bagamoyo.Sambamba na zawadi za waliopendeza pia kutakuwa na zawadi kwa atakayejibu swali la usiku huo ambaye  atajipatia fedha taslimu.

Kimenya amewahakikishia wapenda taaluma na burudani kuwa usiku huu umeandaliwa kwa umakini mkubwa,hivyo wategemee tulizo la mioyo yao kwa kuwa kwenye mikono salama ya waandaji na kupata burudani ya kihistoria katika mji wa Bagamoyo.

Usiku wa Bagamoyo intercolleges night ni usiku wa taaluma na burudani wenye lengo la kuwaunganisha na kuwaburudisha wanavyuo wa mji wa Bagamoyo na nje ya Bagamoyo.Pamoja na burudani wanavyuo watapata nafasi ya kuelezea na kujadili juu ya umuhimu wa kozi wanazojifunza kwa jamii.

No comments:

Post a Comment