Wednesday, November 30, 2011

CUF KUKUTANA NA RAIS KIKWETE


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ofisi ya Rais, Ikulu, imepokea barua kutoka Chama cha Wananchi (CUF) kikiomba kukutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.

Mheshimiwa Rais amekubali ombi hilo la CUF na ameelekeza maandalizi ya mkutano huo yafanyike mara moja.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

30 Novemba, 2011

TAARIFA YA IKULU KUHUSU SALAMU ZA UHURU WA TANZANIA BARA


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Marekani Mheshimiwa Barak Obama ametuma salamu za pongezi na za kuitakia baraka Tanzania wakati inapoadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Tanzania Bara inatimiza miaka 50 ya Uhuru Ijumaa ya wiki ijayo, Desemba 9, 2011.

Aidha, Rais Obama ameihakikishia Tanzania kuwa Marekani itaendelea kubakia rafiki na mshirika wa kuaminika katika jitihada za kuhakikisha kuwa Watanzania kujiletea maisha bora na kwa njia za amani.

Katika salamu zake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais huyo wa Marekani ametumia lugha ya Kiswahili kuitakia baraka Tanzania akimwandikia Mheshimiwa Kikwete, “Mungu awabariki” na kufuatiwa na tafsiri ya maneno hayo hayo katika lugha ya Kiingereza.

Katika salamu zake, Rais Obama ameongeza kuwa umbali mkubwa wa kijiografia kati ya Tanzania unazidi kupungua kwa sababu ya uhusiano wa karibu kati ya Wamarekani na Watanzania.

Amesisitiza Rais Obama, “Hali ya kuwa anuwai ya taifa lako, kama ilivyo ya kwetu, ni chimbuko na msingi wa nguvu zitakazoipitisha Tanzania katika mabadiliko mengi na changamoto nyingi zinazokabili nchi yenye demokrasia inayopanuka.”

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

30 Novemba, 2001

PROF. WANGWE AZINDUA RIPOTI YA TECHNOLOGY AND INNOVATION 2011


Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA Prof. Samuel Mwita Wangwe akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Teknolojia Mbadala ya Mwaka 2011 ambapo amehoji tunawezaje kupunguza umaskini katika kipindi hichi tunachokabiliwa na mabadiliko ya hali ya hewa na ongezeko la Joto Duniani.
Zaidi ya Asilimia 20 ya idadi ya watu Duniani ambao ni sawa na watu Bilioni 1.4 ambao hawana uwezo wa kupata Nishati hiyo wengi wao wakiwa wanaishi Kusini mwa Bara la Asia na Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA Prof. Samuel Mwita Wangwe akizindua TECHNOLOGY AND INNOVATION REPORT2011 ambayo inazungumzia POWERING DEVELOPMENT WITH RENEWABLE ENERGY TECHNOLOGIES.
Na kutoa msisitizo kwa Serikali kuzifanyia kazi ripoti zinazotolewa na wataalamu kwa manufaa ya Taifa kwa ujumla.
The UNCTAD report is available on www.unctad.org

MZEE DAVID WAKATI AMEFARIKI DUNIA


Mtangazaji wa siku nyingi na mwaasisi wa Shirika la Utangazaji la Tanganyika Broardcasting Cooparation (TBC) enzi hizo, na Radio Tanzania Dar es salaam (RTD) Mzee David Wakati amefariki dunia usiku wa kumakia leo. Habari zaidi na mipango ya mazishi tutaendelea kuwajulisha kwa yale yatakayojiri kuhusiana na msiba huo mkubwa kwa wanataaluma ya habari. Mzee David Wakati alikuwa ni mtangazaji mahiri na aliyeitangaza vyema Tanzania katika masuala ya habari kimataifa hasa alipokuwa akifanya kazi katika Idhaa ya Kikwashili ya Sauti ya Ujerumani jijini Born Ujerumani. Mungu aiweke roho ya marehemu David Wakati mahali pema peponi AMEN

KUACHISHWA URATIBU,UJUMBE NA UTENDAJI NDUGU SHABANI MPALULE




 Bodi ya wakurugenzi ya Miss Tourism Tanzania Organisation, yenye dhima ya kikomo ya kuandaa na kuendesha mashindano ya Miss Utalii Tanzania,imeendelea na safisha safisha ya viongozi na waandaaji wababaishaji na mamluki,baada ya kuwafutia kuwatimua waandaaji wa Miss Utalii Dodoma, imemfukuza aliyekuwa mpiga picha wa mashindano hayo katika kamati ya Taifa ya Miss Utalii Tanzania, Shaabani Mpalule,kwa tuhuma za umamluki na hujuma za mashindano hayo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyo tolewa na Rais wa Mashindano hayo, Gideon Chipungahelo, sababu za kufukuzwa ikiwa ni mara ya tatu sasa,baada ya kuwa amefukuzwa mwaka 2008, na kurejeshwa mwaka 2011 mwanzoni na kufukuzwa mwezi July 2011, kisha akaomba msamaha na kurejeshwa mwezi septemba 2011 kwa majaribio.
Sababu za kufukuzwa ni pamoja na utovu wa nidhamu ulio tukuka,kokosa uaminifu, na umamluki wa kuhujumu shindano la Miss Utalii Tanzania. Baadhi ya utovu huo wa ni dhamu na maadili ni pamoja na tuhuma za kutaka kubaka washiriki, kuiba nyaraka za kampuni, kutumia jina la mashindano kujipatia huduma ,mali na hata fedha kwa maslahi binafsi. Kupigana na waandaaji na wanakamati kiasi cha kuharibu mali za watu na hoteli, kuiba mali za wajumbe na wanalamati wengine zikiwemo kamera na mashine za DVD.
Pia imethibitika kuwa ni mamluki ambaye anamaslahi na anatumiwa na waandaaji wa mashindano mengine hususani shindano la Miss Demokrasia ambalo,amekuwa akijaribu kuliandaa bila ya mafanikio, pamoja na hujuma nyingine amekuwa akisambaza mbalimbali za kutengeneza katika mitandao mbalimbali,wadhamini na hata baadhi ya vyombo vya habari ,kutishia warembo na hata kutoa vitisho mbalimbali kwa waandaaji wa ngazi za chini na wanakamati wengine. Aidha amekuwa kinara wa uvurugaji mashindano haya kwa kusambaza taarifa mbalimbali za kukashfu,kucha shindano na kuwachafua viiongozi ,washiriki,washindi na hata sanaa ya urembo na ustawi wa shindano hili na mengine nchini, Wakati wote akiwa mpigapicha wa mashindano haya amekuwa akitumia picha kuwatishia washiriki na kuwapa masharti ambayo ni kinyume cha maadili ili awepe picha. Wakati wote amekuwa na tabia za kutumia au kuweka maelezo tofauti na picha za matukio mbalimbali ya mashindano kwa lengo la kuchafua warembo na mashindano kwa ujuma.
Amefukuzwa kuanzia 21/11/2011, barua yenye sababu za kufukuzwa kwake imeambatanishwa

Pinda azindua Kiwanda cha Serengeti mjini Moshi

 Waziri Mkuu Mizengo Pinda,  jana amezindua kiwanda cha Bia cha Serengeti tawi la Moshi mkaoni Kilimanjaro. Kinwanda hicho cha kisasa na kikubwa kipo eneo la Pasua Boma Mbuzi katika barabara ya Sukari.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mmoja wa Wanahisa wa SBL, Christopher Gachuma mara baada ya kuwasili kiwandano hapo.
Pinda akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL, Teddy Mapunda.
Pinda akisalimiana na Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Ephraim Mafuru
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kiwanda cha SBL mjini Moshi.
Pinda akifunia kitambaa katika moja ya shughuli za uzinduzi wa mjini mosha. Pamoja nae ni Mwenyekiti wa Badi ya SBL, Jaji Mark Bomani na kati kati yao ni Mkuu wa Moa wa Iringa, Leonidas Gama.
Waziri Mkuu akipata maelezo juu ya uzalishaji wa Kiwanda hicho
Pinda akitembezwa katika maeneo mbalimbali ya Kiwanda.
Sehemu ya ujazaji kinywaji cha Serengeti katika kiwanda hicho.
Akiendelea kupata maelezo ya uzalishaji.
 
chanzo father kidevu

KILIMANJARO STARS YAITANDIKA DJIBOUTI MABAO 3:0


HATIMAE KILIMANJARO STARS IMEFANIKIWA KUPATA USHINDI WA KWANZA KWENYE MASHINDANO YA CECAFA TUSKER CHALLENGE CUP 2011 BAADA YA KUIFUNGA DJIBOUTI MABAO 3-0 HAPO JANA KWENYE UWANJA WA TAIFA YANAPOENDELEA MASHAINDANO HAYO.

MABAO HAYO YAMEFUNGWA NA THOMAS ULIMWENGU,MWINYI 
KAZIMOTO NA YUSUF RASHID.

WAKATI HUO HUO RWANDA IMEIFUNGA ZIMBABWE MABAO 2-0 KWENYE MCHEZO ULIYOANZA MAPEMA JANA.

DROGBA AKATAA KUSAINI MKATABA MPYA NA CHELSEA - KUONDOKA MWISHONI MWA MSIMU




Didier Drogba yupo tayari kuondoka Chelsea baada ya kukataa kusaini mkataba mpya.

mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 33, yupo katika siku za mwisho mwisho za mkataba wake unaomuingizia £120,000 kwa wiki na amekataa nyongeza ya miezi 12 katika mkataba wake.

Sasa anajiandaa kuondoka Stamford Bridge akiwa huru kipindi kijacho cha kiangazi kuelekea Russia au Qatar.

Agent wa Drogba Thierno Seydi, alisema jana usiku: “Didier alipewa ofa ya mkataba wa mwaka mmoja na Chelsea. Lakini ameona haumfai.

“Tunajua nini tunataka, wapi tunataka kwenda na kwa ofa ya namna gani. AC Milan walikuja na dili la mkopo kwa Didier wakiwa na option ya kumnunua pia, lakini niliwaambia haiwezekani. Ofa yao haikutuvutia.

“Kwa umri huu wa Didier, hana kipya cha ku-prove kama mchezaji. Ataenda mahala ambapo watatoa mkwanja mrefu zaidi. Inaweza kuwa Marekani , Russia, Qatar au popote in Asia.

“Unapokuwa tayari katika umri wa miaka ya 30 unatakiwa uende katika timu ambayo una uhakika utapata pesa ya kuweza kukuwezesha kuishi vizuri. LA Galaxy ni moja ya timu ambazo Drogba anaweza kujiunga nazo. Pia Anzhi, wanalipa vizuri lakini sio mimi wala Didier tumepokea ofa kutoka kwa timu hizo.”

Drogba alisajiliwa na Jose Mourinho kutoka Marseille kwa ada ya £24million in 2004 na amefunga magoli 146 katika kipindi cha miaka 7 aliyokaa Chelsea.

Habari za Drogba kutaka kuondoka zimekuja siku chache baada ya mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Marcel Desailly kusema kwamba klabu hiyo sasa imegawanyika chini ya Andre Villas Boas, timu haina umoja.

JAMII NI LAZIMA ITAMBUE UMUHIMU WA FANI YA UKUTUBI


Na Aisha Kitupula

NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mh. Philip Mulugo amesema kuwa jamii ni lazima itambue umhimu wa fani ya Ukutubi kwani ni fani ambayo inasaidia kupasha habari jamii na wasomi  kwani kuna  tatizo kwa wananchi wengi kutoifahamu vyema  fani ya Ukutubi kama fani moja muhimu sana katika Sekta ya Elimu na uelimishaji mahali popote Duniani kwani taaluma ya Ukutubi ina historia sawa na kuwepo  na binadamu  kujua wapi alipotoka, alipo na anapokwenda .

Hayo yalisemwa na Mh. Mulugo ambaye ni  Mbunge wa Wilaya ya Songwe Mkoa wa Chunya  katika mahafali ya 17 yaliyofanyika siku ya jumamosi iliyopita ya tarehe 26.11.2011 katika Chuo cha Ukutubi Na Uhifadhi Nyaraka (SLADS) kilichopo Bagamoyo wilaya ya Pwani ambapo alikuwa mgeni rasmi.

Akizungumza katika Mahafali hayo Mh. Mulugo alisema kuwa Ukutubi ni moja ya fani kongwe na inayomgusa kila mtu hasa kwa wasomi katika ulimwengu wa sasa kwani huwasaidia kupata taarifa mbalimbali  zinazohusu masomo na taaluma kwa ujumla hivyo ni lazima kwa kila shule na vyuo ni lazima viwe na maktaba.

“Natambua  umuhimu wa maaktaba ndo maana  Serikali kupitia TAMISEMI ipo katika mchakato wa kuanzisha maktaba za wilaya katika Wilaya yote na hadi sasa baadhi ya Wilaya ikiwemo Wilaya  ya Nachingwea, Korogwe, Ruhangwa na wilaya yangu  ya Chunya wameshaanza kushughulikia  na hadi kufikia tarehe17 disemba wilaya yangu maktaba ya wilaya itakuwa imeshakamilika“  alisema  Mh. Mulugo

Aliongeza kuwa katika kwa hatua kubwa ya kielimu iliyofikiwa na Taifa letu na kuongezeka kwa shule za msingi na sekondari , vyuo na taasisi mbalimbali ni ishara kuwa nafasi za ajira nazo zimeongeza na ongezeko hilo limepelekea kuwepo na taarifa nyingi zitokanazo na tafiti mbalimbali zinazofanywa na wasomaji wengi.

Sote tunafahamu ulimwengu wa sasa ni wasayansi na teknolojia kwani wahitimu wamejifunza nyenzo z kisasa za upashanaji habari (ICT) ninaamini chuo chenu hakijabaki nyuma katika hili na  ni jukumu lenu kukusanya taarifa hizi kuziratibu , kuzichambua na kuziweka katika mifano itayorahisisha utumiaji wake ili zisaidie kuliletea maendeleo Taifa letu. alisema Mh.. Mulugo

Naye Mkuu wa Chuo Bw.Hermenegild  Maganja alisema kuwa hadi kufikia mwaka huu Chuo kimepokea wanafunzi  841 ni namba kubwa tangu kuanziswa kwa chuo hichi mwaka 1989 hii inaonekana wazi kuwa Fani ya Ukutubi imezidi kupiga hatua ingawaje kuna changamoto ya kianzishwa kwa fani hii katika vyuo mbambali ikiwemo SUA, Mzumbe na vingine.

Bw. Maganja kutokana na ongezeko la wanafuzi hao chuo kimekumbana na changamoto mbalimbali ikwemo uhaba wa madarasa , maktaba , usafiri kwa wana chuo, vifaa vya kufundishia hii inatokana na ufinyu wa bajeti kwani chuo kinategemea ruzuku ya Bodi ya Maktaba  Tanzania hivyo chuo kinaomba msaada wa ruzuku kutoka Serikalini kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

RAIS KIKWETE ATIA SAINI MUSWADA WA MABADILIKO YA KATIBA WA MWAKA 2011

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumanne, Novemba 29, 2011, ametia saini Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011.

Hatua hiyo ya Mheshimiwa Rais kutia saini Muswada huo inakamilisha safari ya kutungwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011 baada ya Bunge kuwa limepitisha Muswada huo uliowasilishwa na Serikali katika kikao kilichopita cha Bunge.

Aidha, kutiwa saini kwa Muswada huo ili uwe Sheria ni hatua kubwa na muhimu katika safari ya kutungwa kwa Katiba mpya ya Tanzania kama ilivyoahidiwa na Mheshimiwa Rais Kikwete katika salamu zake za Mwaka Mpya kwa wananchi Desemba 31, mwaka jana, 2010.

Pamoja na kutiwa saini hiyo bado Serikali itaendelea kusikiliza maoni na mawazo ya wadau na wananchi mbalimbali kuhusu namna ya kuboresha sheria hiyo.

Hivyo, Mheshimiwa Rais Kikwete anatoa wito kwa mwananchi yoyote mwenye maoni ama mawazo ya namna ya kuboresha Sheria hiyo, ajisikie yuko huru kutoa maoni yake na Serikali itasilikiza na kuchukua hatua zipasazo.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

29 Novemba, 2011

Tuesday, November 29, 2011

MAHAFALI YA 17 YA CHUO CHA UKUTUBI NA UHIFADHI WA NYARAKA(SLADS )KWENYE PICHA

 Mgeni rasmi wa mafahali bw .Philipo Mulugo naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi(wapili waliyoketi kutoka kushoto mwenye joho jekundu) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa chuo hicho mara baada ya kukamilisha shughuli ya kutunuku vyeti wahitimu wa ngazi ya stashahada na cheti kwa kozi ya ukutubi na uhifadhi wa nyaraka kwenye mahafali ya 17 iliyofanyika kwenye viwanja vya chuo hicho mijini bagamoyo jumamosi iliyopita ya tarehe 26.11.2011.Kushoto kwa mgeni rasmi ni mwenyekiti wa bodi wa chuo hicho Dkt.Ally Mcharazo,kulia mwa mgeni rasmi ni Mkuu wa chuo bw.Hermenegild Maganja na kulia kabisa ni bi.Happiness Steven Mkuu wa taaluma wa chuo hicho.Waliyosimama nyuma ni wafanyakazi wa chuo hicho(SLADS).
 Mkuu wa taaluma bi. Hppiness Steven akitangaza jambo wakati wa mahafali hiyo.
 Wahitimu wa ngazi ya cheti wakisubiri kauli ya mgeni ya kuwatunuku vyeti.
 Wahitimu wa ngazi ya cheti wakivaa kofia kuashiria kutunukiwa vyeti.
 Wahitimu wa ngazi ya stashahada mara baada ya kutunukiwa vyeti.
 Mdau Felister mara baada ya kutunukiwa stashahada.
 Mdau Manka mara baada ya kutunukiwa stashahada.
 Mdau Sophia mara baada ya kutunikiwa stashahada.
 Mdau Rahma kulia mara baada ya kutunikiwa cheti.Kwa sasa Rahma ni mwanachuo wa SLADS kwa ngazi ya stashahada.
 Mkurugenzi wa kampuni ya kimkev entertainment bw.Kim Kimenya kushoto akiwa miongoni mwa wageni waliyohudhurria mahafali hiyo.
Mdau James Telekako mara baada ya kutunukiwa cheti.Kwa sasa James ni mwanachuo wa SLADS kwa ngazi ya stashahada.
 Mc Mitti mwanachuo wa zamani wa chuo hicho akiwa miongoni mwa wahudhuriaji wa mafahafali hiyo.Kwa sasa Mitti yupo chuo cha usimamizi wa fedha I.F.M kama mtumishi.
Kamati ya maandalizi ya mafahafali ikiwa kazini.mdau Kingu waziri wa ulinzi wa SLADSO akiwa katikati.

Monday, November 28, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA SIKU WA VIONGOZI WA TAKUKURU-TANGA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Takukuru, Edward Hosea, baada ya kufungua rasmi mkutano Mkuu wa mwaka wa Viongozi wa Takukuru uliofanyika Mkoani Tanga leo Novemba 28, 2011. Picha na Muhidin Sufiani-OMRi

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Takukuru, Edward Hosea, mara baada ya kufungua ramsi mkutano Mkuu wa mwaka wa siku mbili wa Viongozi wa Takukuru uliofunguliwa leo Novemba 28, mkoani Tanga. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Viongozi wa Takukuru Mkoani Tanga leo Novemba 28. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Takukuru, Edward Hosea (kushoto) ni Waziri wa Ofisi ya Rais-Utawala Bora, Mathias Chikawe. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Viongozi wa Takukuru Mkoani Tanga leo Novemba 28. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Takukuru, Edward Hosea (kushoto) ni Waziri wa Ofisi ya Rais-Utawala Bora, Mathias Chikawe. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

ANTVIRUS SHOW ILIVYOJILI VIWANJA VYA USTAWI JUZI


FULL MZUKA HAKUNA ALIEFUNIKWA JUZI SUGU NA FABOLOUS NGOMA DROO

ST8 MUZIK NDANI YA LEADERS 2011


Mwanamuziki wa hip hop toka nchini Marekani Fabolous akikamua kwenye tamasha hilo lililo hapen katika viwanja vya Leaders jijini Dar na kuhudhuriwa na bonge la nyomi
Msanii wa Hip hop toka bongo land Jay Mo akikamua sanjari na mwana hip hop mwenzie Mchizi Mox

Simba mzee, Mfalme asiyevuliwa taji Selemani Msindi aka Afande Sele alikosha kisasawa mashabiki walo hudhuria tamasha hilo.
Masoja Long time kitambo wanaitwa Gangwe Mobb.

WAREMBO WAWILI MISS UTALII TANZANIA 2010/2011 KWENDA UTURUKI DISEMBA 19 2011








Mshindi wa tano wa fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania2010/2011 Sophia Dio na mshindi wa taji la vipaji la Miss Utalii Tanzania 2010/2011 Dessy Mushumbuzi,wanatarajia kuondoka nchini 19-12-2011 ,kwenda kuwakilisha Tanzania katika mashindano ya Dunia ya Miss Globe International 2011.

Jumla ya nchi 120 Duniani zinashiriki katika shindano hilo,litakalofanyika 30-12-2011 katika jiji la Istanbul na kuonyeshwa Live kupitia TV mbalimbali Duniani. Shindano hilo kama lilivyo shindano la Miss Utalii Tanzania,linalenga kutangaza na Utalii,Utamaduni wa mataifa mabalimbali Duniani,pia kuunganisha na kubadilishana tamaduni miongoni mwa mataifa na washiriki.


Hii itakuwa ni fulsa nyingine kwa Tanzania kuweza kutangaza utalii na utamaduni wetu kimataifa, na hata mianya ya uwekezaji iliyopo Tanzania kupitia warembo hawa wa Miss Utalii Tanzania, ambao historia inaonyesha kuwa mara zote wanaposhiriki mashindano ya Dunia na kimataifa hutwaa mataji mbalimbali. hadi sasa Miss Utalii Tanzania tunashikilia zaidi ya mataji 5 ya Dunia,yakiwemo Miss Tourism World 2005- Africa, Miss Tourism World 2006 -SADC, Miss Tourism World 2007 - Africa, Model Of The World 2008 - Personality , Miss Africa 2006 - !ST Runner Up n.k


Tunaendelea na maandalizi kuhakikisha tunadumisha na hata kuvuka rekodi ya kwa kuahalilisha kuwa warembo hao wanarudi na mataji na sio wasindikizaji kama walivyo wengine. Tunaomba makampuni na watu mabalimbali wajitokeze kudhamini na kuchangia safari na ushiriki wa warembo hao katika mashindano hayo ya Dunia