Monday, November 21, 2011

MATUKIO YA PICHA RAIS KIKWETE AKIONGEA NA WAZEE WA DAR ES SALAAM KWENYE UKUMBI WA (PTA)


Rais Jakaya Kikwete akiongea na wazee wa mkoa wa Dar es salaam hivi jioni hii kwenye ukumbi wa PTA viwanja vya maonyesho vya Mwalimu J.K.Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam. Rais Kikwete anazungumzia masuala mbalimbali yakiwemo mamasuala ya kiuchumi na masuala ya mchakato wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wazee mbalimbali wa chama na wastaafu wamekusanyika katika ukumbi huo ili kusikiliza na ambapo mambo mbalimbali watakayoambiwa,ili nao pia waweze kufikisha ujumbe kwa wanzao ambao hawajapata nafasi ya kuhudhuria katika mkutano huo na wananchi kwa ujumla Wazee wa jiji la Dar es salaam wakimsikiliza Rais Dk. Jakaya Kikwete wakati alipoongea nao katika ukumbi wa PTA barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam leo jioni.
Rais Jakaya Kikwete akiwasilia kwenye ukumbi wa PTA tayari kuongea na wazee wa Dar es salaam pamoja na wananchi kwa ujumla, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dare salaam Meck Sadick na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam.
Rais Jakaya Kikwete akiongoza viongozi wa mbalimbali na wazee wa Mkoa wa Dar es salaam kumkumbuka mmoja wa wazee wa CCM ambaye alikuwa kiongozi katika baraza la wazee katika picha kutoka kulia ni Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Meck Sadick na kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam John Guninita na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Dar es salaam Brigedia Mstaafu Hashim Mbita.
Kutoka kulia ni Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam John Guninita katikati na Mkuu wa wilaya Mstaafu mama Hawa Ngulume wakijadiliana jambo kabla ya Rais kuwasili katika ukumbi huo
Wazee mbalimbali wakiwa wamekusanyika kwenye ukumbi wa PTA tayari kwa kumsikiliza Mh. Rais Jakaya Kikwete.
Hapa wakionekana kujadiliana mambo kadhaa kabla ya Rais kuwasilia katika mkutano huo jioni hii.Baadhi ya wazee kutoka mtoni Wilayani Temeke wakiwa katika ukumbi huo kwa ajili ya kumsikiliza Mh. Rais Jakaya Kikwete.

No comments:

Post a Comment