Wednesday, November 16, 2011

Mchezo wa Marudiano Taifa Stars Vs Chad; Wao Moja sisi Bila. Stars yasonga


Mchezaji wa timu ya Taifa Stars Mbwana Samatta kulia akichuana na beki wa timu ya taifa ya Chad Yaya Karim katika pambano la timu hizo linaloendelea kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuwania kufuzu kombe la dunia nchini Brazil mwaka 2014, Stars inahitaji kushinda au kutoka Droo yoyote ili kusonga mbele na mpaka mpira umekwisha nacha timu ya Chad imeshinda kwa goli1-0 dhidi ya Taifa Stars. Hata hivyo Taifa stars inasonga mbele na kwa shria ya magoli ya ugenini na kuingia hatua ya makundi kwa magoli ambapo kwa matokeo ya leo ina maana taifa Stars inasonga mbele kwa ushindi wa 4-3
Hekaheka katika lango la timu ya Chad kama linavyoonekana hapa.
Kikosi cha timu ya Chad kikiwa katika picha ya pamoja.
Mashabiki wa timu ya Taifa wakiimba wimbo wa taifa kabla ya pambano hilo.
Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti SBL Ephraim Mafuru wa pili kutoka kushoto na Mkurugenzi wa Mawasiliano SBL Teddy Mapunda wakijadili jambo na kabla mpira haujaanza.
Msanii huyu wa ngoma akitoa burudani wakati wa mapumziko ya timu hizo kwenye uwanja wa Taifa.
Kamanda Misime wa polisi Mkoa wa Temeke akizungumza na Mkurugenzi wa Mawasiliano SBL Teddy Mapunda, kabla mpambano huo haujaanza kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jioni jana.  Picha na Fullshangwe Blog

No comments:

Post a Comment