Wednesday, November 16, 2011

Kambi ya Upinzani Bungeni yasusia Bunge, ni wakati wa kusomwa mara ya pili muswada wa Katiba


Na mwandishi maalumu
Kambi  rasmi ya upinzani ikiongozwa na kiongozi wake, Mh Freeman Mbowe jana  imetoka nje ya ukumbi wa Bunge mara tu baada ya kuwasilishwa kwa mara ya pili kwa muswada wa kuundwa kwa tume ya kusimamia uundwaji wa katiba mpya.

Wabunge hao ambao kwa siku ya jana wameungwa mkono na wabunge wa NCCR-Mageuzi, David Kafulila na Felix Mkosamali waliamua kutoka nje kwa kile walichokiita kunyanyaswa na spika.

Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kutoka ukumbini, kiongozi wa kambi ya upinzani, Bwana Freeman Mbowe alisema wapinzani wamefikia hatuia hiyo baada ya kugundua kiburi, dharau na upendeleo wa wazi aliouonesha Spika wa bunge, Bi Ana Makinda dhidi ya wabunge wa upinzani.

“ Tumeamua kutoka bungeni baada tya spkia kuoneshawaziwazi kuwa anaitetea serikali, amekataa kuwaruhusu wapinzani kuomba miongozo na ddhahiri ameonesha dharau kwa kusema tunapoteza muda,” amesema Mbowe.

Awali mbunge wa Ubungo, Bw. John Mnyika, Mbunge wa Muhambwe, Bw. Felix Mkosamali na Mbunge wa Maswa, Bw. John Shibuda kwa nyakati tofauti walinyanyuka na kuomba miongozo ya spka lakini spika hakuwa tayari kuwapatia nafasi ya kuongea nabadala yake alimruhusu Mbunge wa Same, Bi Ana Kilango kuanza kutoa mchango wake.

Akielezea suala hilo, Mbunge wa Mhambwe, Bwa Felix Mkosamali ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya katiba Bungeni alieleza kuwa Spika amekuwa mwiba mkali kwa kuburuza kamati hiyo iliyopewa dhamana ya kukusanya maoni ya wananchi juuya uundajiwa katiba mpya.

Kwa mujibu wa Mkosamali, mpaka muswada huo unaletwa Bungeni, wajumbe wa kamati hiyo walikuwa wametofautiana na kwamba mwenyekiti wa kamati, Bi Pindi Chana alilazimishwa na Spika kuleta muswada Bungeni.

Hata hivyo kambi rasmi ya upinzani imeapa kutohudhuria vikao vyote vya mjadala unaohusu kupitishwa kwa muswada wa uundwaji wa Katiba mpya huku ikidai kuusoma muswada huo mara ya pili ni kinyume na matakwa ya Watanzania.

No comments:

Post a Comment