Sunday, November 13, 2011

TIMU NA RATIBA YA KOMBE LA CECAFA TUSKER CHALLENGE YATANGAZWA




Katibu Mkuu wa Shirikisho la vyama vya michezo Afrika Mashariki CECAFA Nicholas Musonye akizungumza na waandishi wa habari asubuhi ya jumatano iliyopita katika hoteli ya New Africa, wakati akitangaza timu zitakazoshiriki katika mashindano ya CECAFA Tusker Challenge Cup 2011 yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni nchini, wanaofuatia katika picha ni Leodger Tenga Rais Mwenyekiti wa CECAFA na Rais wa TFF, Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mahusiano SBL na Ritha Chaki Meneja wa Kinywaji cha Tusker.
Waandishi mbalimbali wa habari wakiwa katika mkutano huo.
 
Kampuni yabia ya Serengeti wakishirikiana na Shirikisho la mpira wa miguu Africa Masharikin a Kati (CECAFA) leolimetoa ratiba ya michuano ya kombe la CECAFA Tusker Challenge 2011 linalotarajiakutimuavumbikuanziaNovemba 25 hadiDisemba 10 hapa Tanzania. 

KatibuMkuuwa CECAFA Nicholas Musonye alitangaza ratiba ya makundi katika mkutano na waandishi wahabari ulioandaliwa na kampuni ya bia ya Serengeti,na kufanyika jijini Dar es Salaam jumatano iliyopita. Mkutano huo pia ulihudhuliwa na ujumbe kutoka TFF, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Bi Teddy Mapundana Meneja wa biayaTusker Bi. Rita Mchaki. 

Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia bia yake yaTusker ni mdhamini mkuu wa michuano hiyo ambapo imetoa kiasi cha Shilingi milioni 823. Takribani timu 11 zitashiriki michuano hiyo zikiwemo timu ya Malawi ambao watacheza kwamwaliko maalum.

“Tumeialika timu hii makusudi kwa nia ya kusisimua maendeleo ya soka katika ukanda huu. Ni matumaini yetu kuwa timu hii italeta changamoto katikamichuano hiyo na kuifanya iwe na ushindani mkubwa,” Musonye amekaririwa akisema.

Bw. Musonye aliendelea kusema kwamba, ’niLengo la CECAFA kuona mpira wa miguu katika ukanda huu unakuwa wa kiwango cha juu kabisa. Na timu mojawapo katika ukanda huu ituwakilishe katika mashindano ya mpira wa miguu Tanzania 2014 huko Brazil’.
Akiongezea hayo, kwa msisitizo Bi Teddy Mapunda, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti alisema kwambaiudhamini huu ni mojawapo wa jitihada za kampuni ya SBL katika kuinua kiwango cha soka kanda hili.

Kwa Upande wake, Meneja wa bia ya Tusker, Rita Mchaki aliwahamisha watanzania wajitokeze kwa wingi na wawe tayari kuburudika, kwani kupitia bia ya Tusker, mechi za CECAFA mwaka huu zitakuwa na mengi. Kutakuwa na burudani kila siku uwanjani, kinywaji bora cha Tusker kitapatikana ndani na pia zawadi kem kem kushindaniwa. Pia alikumbusha wananchi kuwa kiingiliio kitakuwa sawa na bure.

Mwaka huu, timu zitakazoshiriki ni kutokaKenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Djibouti, Somalia, Ethiopia, Sudan, Tanzania, Zanzibar, Eritrea.

Kampuni ya bia ya Serengeti inapata heshima ya kuwa mdhamini mkuu na kupata hakimiliki ya kutumia nafasi hii kutangaza bidhaa yaTusker kipindi chote cha mashindano haya.

No comments:

Post a Comment