Tuesday, November 8, 2011

ZANZIBAR HEROES YAPEWA VIFAA


Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Future Century Ltd, Hellene
Masanja (kushoto) na kocha wa timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar
Heroes, Stewart Hall wakiangalia moja ya jezi zilizokabidhiwa na
kampuni hiyo kwa ajili ya maandalizi ya Zanzibar Heroes katika
mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na kati (CECAFA). Hafla
hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo. Wa pili Kulia ni Nahodha
Msaidizi wa Heroes, Nadir Haroub ‘Canavaro’ na Mjumbe Kamati Tendaji
ya Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), Abdalla Thabit Juma.  Zanzibar
Heroes inatarajiwa kuondoka jijini humo kesho kuelekea Misri kucheza
mechi za majaribio za kimataifa kama sehemu ya maandalizi hayo.


Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Future Century Ltd, Hellene
Masanja (kushoto) akikabidhi jezi, viatu na vifaa vingine vya michezso
kwa kocha wa timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes, Stewart Hall
(wa pili kulia) na Nahodha Msaidizi wa Heroes, Nadir Haroub ‘Canavaro’
(kulia) kwa ajili ya maandalizi ya timu hiyo katika mashindano ya
Klabu Bingwa Afrika Mashariki na kati (CECAFA). Hafla hiyo imefanyika
jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mjumbe Kamati Tendaji ya Chama
cha Soka Zanzibar (ZFA), Abdalla Thabit Juma.  Heroes inatarajiwa
kuondoka jijini humo kesho kuelekea Misri kucheza mechi za majaribio
za kimataifa kama sehemu ya maandalizi hayo.

No comments:

Post a Comment