Thursday, November 3, 2011

SERENGETI YATOA MIL 823 KWA CECAFA TUSKER CHALLENGE CUP


Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya mpira wa miguu Afrika Mashariki (CECAFA) Nicolas Musonye (kulia), akipokea mfano wa cheki yenye thamani ya shilingi milioni 823 kutoka kwa Richard Wells Mkurugenzi wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) katika mkutano uliofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam asubuhi hii, katikati ni Jaji Mark Bomani Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL).


Mkurugenzi wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Richard Wells akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa (CECAFA) wakati alipotangaza udhamini wa shilingi milioni 823 kwa ajili ya mashindano ya Tusker Challenge Cup 2011 yatakayofanyika jijini Dar es salaam hivi karibuni, wanaofuatia katika picha ni Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano (SBL) na Ritah Mchaki Meneja wa kinywaji cha Tusker.
Mkurugenzi wa Mawasiliano (SBL),Teddy Mapunda akizungumza leo asubuhi kuhusiana na kutanganza udhamini wao wa kombe la mashindano ya CECAFA Tusker Challange Cup 2011 mwaka huu,kupitia bia yake ya Tusker,kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa SBL,Richard Wells.Teddy aliongeza kuwa Udhamini huu ni wa kiasi cha fedha za kitanzania shillingi milioni 823. Fedha hizi zitagharamia mahitaji kama vile: tiketi za ndege kwa msafara wote wa CECAFA pamoja na wahusika wakuu wa CECAFA, malazi, usafiri wa magari hapa nchini, watoa huduma, fedha za washindi, malipo ya CECAFA ndani na nje ya nchi. Kodi ya uwanja wa mpira, ulinzi na sehemu za mazoezi kwa wachezaji. Hali kadhalika, fedha hizi zitatumika kuratibu waandishi wa habari na mahitaji mengine ya utawala. Mashindano haya yanategemewa kuanza tarehe 25 Ocktoba hadi tarehe 10 Disemba 2011.

Mwenyekiti wa CECAFA na Rais wa TFF, Leodger Tenga akifafanua jambo mapema leo asubuhi mbele ya wanahabari kuhusiana na ushiriki wa timu mbalimbali katika mashindano ya CECAFA Tusker Challange Cup 2011,Tenga amezitaja timu zitakazoshiriki mwaka huu kuwa ni kutoka Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Djibouti, Somalia,Ethiopia, Sudan, Tanzania, Zanzibar, Eritrea.Tenga aliongeza kuwa kwa kiasi hicho cha udhamini, kampuni ya bia ya Serengeti inapata heshima ya kuwa mdhamini mkuu na kupata haki miliki ya kutumia nafasi hii kutangaza bidhaa ya Tusker kipindi chote cha mashindano haya.

No comments:

Post a Comment