Wednesday, November 30, 2011

JAMII NI LAZIMA ITAMBUE UMUHIMU WA FANI YA UKUTUBI


Na Aisha Kitupula

NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mh. Philip Mulugo amesema kuwa jamii ni lazima itambue umhimu wa fani ya Ukutubi kwani ni fani ambayo inasaidia kupasha habari jamii na wasomi  kwani kuna  tatizo kwa wananchi wengi kutoifahamu vyema  fani ya Ukutubi kama fani moja muhimu sana katika Sekta ya Elimu na uelimishaji mahali popote Duniani kwani taaluma ya Ukutubi ina historia sawa na kuwepo  na binadamu  kujua wapi alipotoka, alipo na anapokwenda .

Hayo yalisemwa na Mh. Mulugo ambaye ni  Mbunge wa Wilaya ya Songwe Mkoa wa Chunya  katika mahafali ya 17 yaliyofanyika siku ya jumamosi iliyopita ya tarehe 26.11.2011 katika Chuo cha Ukutubi Na Uhifadhi Nyaraka (SLADS) kilichopo Bagamoyo wilaya ya Pwani ambapo alikuwa mgeni rasmi.

Akizungumza katika Mahafali hayo Mh. Mulugo alisema kuwa Ukutubi ni moja ya fani kongwe na inayomgusa kila mtu hasa kwa wasomi katika ulimwengu wa sasa kwani huwasaidia kupata taarifa mbalimbali  zinazohusu masomo na taaluma kwa ujumla hivyo ni lazima kwa kila shule na vyuo ni lazima viwe na maktaba.

“Natambua  umuhimu wa maaktaba ndo maana  Serikali kupitia TAMISEMI ipo katika mchakato wa kuanzisha maktaba za wilaya katika Wilaya yote na hadi sasa baadhi ya Wilaya ikiwemo Wilaya  ya Nachingwea, Korogwe, Ruhangwa na wilaya yangu  ya Chunya wameshaanza kushughulikia  na hadi kufikia tarehe17 disemba wilaya yangu maktaba ya wilaya itakuwa imeshakamilika“  alisema  Mh. Mulugo

Aliongeza kuwa katika kwa hatua kubwa ya kielimu iliyofikiwa na Taifa letu na kuongezeka kwa shule za msingi na sekondari , vyuo na taasisi mbalimbali ni ishara kuwa nafasi za ajira nazo zimeongeza na ongezeko hilo limepelekea kuwepo na taarifa nyingi zitokanazo na tafiti mbalimbali zinazofanywa na wasomaji wengi.

Sote tunafahamu ulimwengu wa sasa ni wasayansi na teknolojia kwani wahitimu wamejifunza nyenzo z kisasa za upashanaji habari (ICT) ninaamini chuo chenu hakijabaki nyuma katika hili na  ni jukumu lenu kukusanya taarifa hizi kuziratibu , kuzichambua na kuziweka katika mifano itayorahisisha utumiaji wake ili zisaidie kuliletea maendeleo Taifa letu. alisema Mh.. Mulugo

Naye Mkuu wa Chuo Bw.Hermenegild  Maganja alisema kuwa hadi kufikia mwaka huu Chuo kimepokea wanafunzi  841 ni namba kubwa tangu kuanziswa kwa chuo hichi mwaka 1989 hii inaonekana wazi kuwa Fani ya Ukutubi imezidi kupiga hatua ingawaje kuna changamoto ya kianzishwa kwa fani hii katika vyuo mbambali ikiwemo SUA, Mzumbe na vingine.

Bw. Maganja kutokana na ongezeko la wanafuzi hao chuo kimekumbana na changamoto mbalimbali ikwemo uhaba wa madarasa , maktaba , usafiri kwa wana chuo, vifaa vya kufundishia hii inatokana na ufinyu wa bajeti kwani chuo kinategemea ruzuku ya Bodi ya Maktaba  Tanzania hivyo chuo kinaomba msaada wa ruzuku kutoka Serikalini kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

No comments:

Post a Comment