Mwandishi wetu
BENDI ya muziki wa dansi ya African Stars “Twanga Pepeta International” itafanya onyesho kwa mara ya pili nchini Uingereza Jumamosi hii.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa kampuni ya Afrikan Stars Enterteinment (ASET), Asha Baraka alisema kuwa jumla ya wasanii 13 wanatarajiwa kwenda huko kwa ajili ya kusherehekea miaka 50 ya Uhuru na Watanzania wahishio huko.
Baraka alisema, wanamuziki wao wanatarajiwa kuondoka Ijumaa na shoo itafanyika Jumamosi kwenye ukumbi wa Silver Spoon, Wembley bendi hiyo ikiwa huko itaendelea kufanya shoo zake kama kawaida nchini.
Mara ya kwanza kwa bendi hiyo kufanya shoo ilikuwa mwaka 2007 ambapo ilifanya shoo kwa wiki tatu katika miji mbali mbali mikubwa duniani.
Alisema, mgeni rasmi katika shoo hiyo anatarajiwa kuwa Balozi wa Tanzania wa Uingereza ambaye ni Peter Kallaghe na maandalizi yanaendelea vizuri ya safari hiyo.
“Kama unavyofahamika kuwa Tanzania tulitawaliwa na Waingereza na huko wapo Watanzania wanaohishi huko tumeona ni vyema tukaenda kuungana nao wenzetu kwa ajili ya kusherehekea miaka 50 ya Uhuru, alisema Baraka.
“Wasanii wanaoenda huko ni 13 na wengine watabaki kuendelea na shoo kama kawaida kwenye kumbi mbalimbali kwenye viwanja vya Leaders tutaungana na Msondo Ngoma,” alisema Baraka.
No comments:
Post a Comment