Tuesday, August 12, 2014

TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2014 LAZINDULIWA KWA KISHINDO JIJINI MWANZA.


Nyota wa  muziki wa bongo fleva, Naseeb Abdul 'Diamond Platinum' akilitawala jukwaa pamoja na baadhi ya wacheza shoo wake katika onyesho  la kwanza la tamasha la Serengeti fiesta katika Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza lililofanyika mwishoni mwa wiki,tamasha hilo litaendelea kwenye miji mingine ya Bukoba na Kahama mwishoni mwa wiki.
 Baada ya kazi ya kuwaburudisha mashabiki wake,Mara Wema Sepetu a.k.a shemeji nae akajiunga kumpa sapoti mpenzi wake jukwaani.
Sehemu ya umati wa wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tamasha la Serengeti fiesta 2014 lililoanza rasmi katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
  Sehemu ya umati wa wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tamasha la Serengeti fiesta 2014 lililoanza rasmi katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
 Diamond na Ney wa Mitego wakioneshana umwamba wa kuwateka mashabiki kila mmoja kwa staili yake,huku miluzi na Shangwe ikiwa imtawala ndani ya uwanja.
 Mmoja wa wasanii anaefanya vyema kwa sasa katika anga ya muziki wa bongofleva Vanessa Mdee a.k.a V Money akitumbuiza mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza (hawapo pichani) waliojitokeza kwa wingi kushuhudia mrindimo wa tamasha la Serengeti Fiesta ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo,tamasha hilo limefanyika mwishoni mwa wiki

No comments:

Post a Comment