Basi la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limekamatwa na madalali kwa amri ya mahakama kutokana na deni la sh milioni 140 ambalo shirikisho linadaiwa na litaachiwa hadi hapo deni litakapolipwa.
Awali TFF ilifanya juhudi kubwa kuficha suala hilo kuhusiana na kukamatwa na basi hilo.
Lakini juhudi za gazeti la Michezo la Championi kufuatilia kwa juhudi, zimelilazimu shirikisho hilo kuweka mambo hadharani.
Katika taarifa iliyotolewa leo na Ofisa Habari wake, Boniface Wambura imeeleza kuwa amri hiyo imetokana na deni hilo la kampuni ya Punchline ya Kenya iliyokuwa ikichapa tiketi za kuingilia uwanjani kuanzia mwaka 2007. Hadi sasa tumeshalipa sh. milioni 70 katika deni hilo.

"Jitihada zinafanyika ili kumaliza deni hilo. Pia tunachunguza mwenendo mzima uliosababisha kuwepo deni hilo," alisema Wambura.
No comments:
Post a Comment