Friday, August 15, 2014

SUAREZ AANZA KUPASHA NA 'MASTAA' WA BARCELONA, KUTAMBULISHWA JUMATATU NA KUSHUKA DIMBANI

 

A work out at last: Luis Suarez trains with his Barcelona team-mates on Friday, including club captain Xavi

Kazi imeanza: Luis Suarez akifanya mazoezi na wachezaji wenzake wa  Barcelona leo ijumaa akiwemo nahodha wa klabu, Xavi.

HATIMAYE Luis Suarez ameanza mazoezi na wachezaji wenzake wa Barcelona baada ya kuruhusiwa na mahakama ya juu ya rufani ya michezo CAS.
Nyota huyo mwenye miaka 27 alifungiwa kucheza mechi za mashindano na FIFA mwezi Julai mwaka huu baada ya kumng'ata beki wa Italia Giorgio Chiellini katika fainali za kombe la dunia.
Adhabu yake ya kifungo cha miezi minne inaendelea, lakini CAS imemruhusu kufanya mazoezi na wachezaji wenzake katika klabu yake mpya.
Suarez alikuwa anajiandaa peke yake kufuatia kusajiliwa kwa paundi milioni 75 kutoka klabu ya Liverpool na kujiunga na miamba ya Katalunya, lakini sasa anajiunga katika mazoezi na Lionel Messi.
All smiles: Barcelona are well under way with their pre-season preparations, while Suarez has been training alone

Tabasamu: Barcelona wanaendelea vizuri kujiandaa na msimu mpya na tayari Suarez amejiangu katika mazoezi 
Fitting in with the Barca style: The former Liverpool striker joins in with keepy-uppies at the training ground

Akijiimarisha na staili ya Barca : Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool amejiunga na wenzake katika mazoezi ya pamoja.

Baada ya CAS kumruhusu Suarez kufanya mazoezi na klabu, sasa Barcelona inaweza kumtambulisha rasmi jumatatu katika dimba la Camp Nou.
Muuruguay huyo sasa anaweza kucheza mechi za kirafiki na atavaa jezi ya Barcelona dhidi ya Leon FC katika mchezo wa kombe la  Joan Gampher kwenye dimba la Nou Camp jumatatu jioni.
Kifungo cha Suarez kimebakia katika mechi 8 za mashindano za Uruguay na atakosa mechi za Copa America mwakani na baadhi ya mechi za kufuzu kombe la dunia.
Lakini mahakama amethibitisha kuwa mchezaji huyo anaruhusiwa kucheza mechi za kirafiki chini ya sheria za nidhamu za FIFA.

No comments:

Post a Comment