Monday, August 11, 2014

SIMBA SC YAVUNJA MKATABA NA LOGARUSIC, MATOLA SASA KUKAIMU NAFASI YAKE


Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
SIMBA SC imevunja Mkataba na kocha wake, Mcroarta Zdravko Logarusic siku moja tu baada ya timu hiyo kufungwa mabao 3-0 na ZESCO ya Zambia katika mchezo wa kirafiki jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Rais wa Simba SC, Evans Aveva amesema kwamba Logarusic amevunjiwa Mkataba kwa kukiuka masharti ya mwajiri wake na sasa Nahodha wa zamani wa klabu hiyo, Suleiman Abdallah Matola ‘Osama’ aliyekuwa Msaidizi wa Loga, ndiye anakuwa kaimu kocha Mkuu hadi atakapopatikana mwalimu mwingine.

Kibarua kimeota magugu; Zdravko Logarusic amefukuzwa Simba SC baada ya miezi 10 
Loga ambaye aliongezewa Mkataba wa mwaka mmoja mwezi uliopita- inadaiwa amefukuzwa kwa sababu za kinidhamu na kikubwa ni kuwatolea maneno yasiyofaa wachezaji.
Inaelezwa Loga alifikia hatua ya kuwadharau na kuwatolea maneno yasiyofaa hadi viongozi wa klabu hiyo.
Loga anaondoka Simba SC baada ya kuiongoza katika mechi 21 tangu Desemba mwaka jana, kati ya hizo akishinda nane, sare tano na kufungwa nane.
Loga aliyerithi mikoba ya Mfaransa, Patrick Liewig aliikuta Simba SC bado ipo kwenye mbio za ubingwa msimu uliopita, lakini mwishowe ikamaliza nafasi ya nne nyuma ya Mbeya City, Yanga SC na Azam FC mabingwa

No comments:

Post a Comment