Tuesday, August 19, 2014

OKWI : SINA MPANGO WA KURUDI BONGO

 

Emmanuel OkwiWAKATI uongozi wa Yanga ukidai hauna muda kuendelea kulijadili suala la mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi, mshambuliaji huyo naye amesema hana mpango wa kurudi kucheza soka Tanzania.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kupitia ukurasa wake wa Facebook, Okwi alisema hana mpango wa kurudi nchini kwa sasa, kwani anachoangalia ni kucheza soka barani Ulaya na sio Tanzania.
Awali, Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu, alikaririwa akisema, wanachoangalia wao kwa sasa ni wachezaji gani wamefika na maendeleo yao katika mazoezi, sio kumfuatilia yule ambaye hajafika.
Okwi inadaiwa kuwa anaidai Yanga zaidi ya sh. milioni 60 zilizotokana na fedha zake za kusajiliwa akitokea Etoile du Sahel ya Tunisia, huku akisaini mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya sh. milioni 160.
Hata hivyo klabu hiyo inatakiwa kuvunja mkataba na mchezaji mmoja wa kimataifa kutokana na kuzidi kwa idadi ya wachezaji watano wa kigeni kama zinavyotaka sheria za usajili wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Wachezaji wengine wa kimataifa waliopo katika klabu hiyo ni Andrey Coutinho, Geilson Santos ‘Jaja’ raia wa Brazil, Mbuyu Twite wa Burundi, Hamis Kiiza wa Uganda na Haruna Niyonzima wa Rwanda

No comments:

Post a Comment