Thursday, August 14, 2014

EBOLA YASABABISHA CAF KUZUIA BAADHI YA MECHI




Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limezuia mechi zake kuchezwa Guinea, Liberia na Sierra Leone kutokana na kuripotiwa kuwepo kwa wagonjwa wengi wa Ebola katika nchi hizo.


Ikiwa ni njia mojawapo ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya ugonjwa huo kupitia mkusanyiko wa watu, CAF imevitaka vyama vya mpira wa miguu vya nchi hizo kuchagua viwanja vingine huru kwa ajili ya timu zao zinazoshiriki michuano yake kwa kipindi hiki hadi katikati ya mwezi ujao.

CAF itafanya tathmini nyingine kuhusiana na ugonjwa huo kuanzia katikati ya Septemba ili kuona kama nchi hizo zinaweza kupokea timu ngeni kwa ajili ya mechi mbalimbali za michuano yake, na baadaye kufanya uamuzi wa kuruhusu au kuendelea kusimamisha.

Pia kutokana na mapendekezo ya Shirika la Afya Duniani (WHO), CAF imesema kwa nchi zenye virusi vya Ebola ni muhimu kwa vyama vyake vya mpira wa miguu kuufanyia vipimo vya afya msafara wa timu zao ili kuhakikisha wenye virusi vya ugonjwa huo hawasafiri.

No comments:

Post a Comment