Monday, August 4, 2014

Miss Tanzania 2012, JAT kusomesha albino 50


 Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango wa kutoa elimu kwa wajasiliamali kwa albino 50, kushoto ni Kaimu katibu Mkuu wa Jumuiya wa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), Mohamed Chanzi.
 
 Kaimu katibu Mkuu wa Jumuiya wa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), Mohamed Chanzi (Kushoto) akisisitiza jambo katika uzinduzi wa mpango huo. Wengine katika picha ni Brigitte Alfred (katikati) na Maria Ngowi ambaye ni mkurugenzi wa JAT
 
Viongozi wa Taasisi ya Brigitte Alfred Foundation, TAS na JAT katika picha ya pamoja mara baada ya kuzinduzi mpango wa kusomesha albino 50 masomo ya Ujasiriamali.
 ***********
Na Mwandishi wetu
Taasisi ya ya Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred ijulikanayo kwa jina na Brigitte Alfred Foundation (BAF) ikishirikiana na taasisi ya Junior Achievement Tanzania (JAT) inazindua rasmi mafunzo ya ujasiriamali kwa jamii ya Albino.
 
Akizungumza katika uzinduzi huo jana, Brigitte alisema kuwa taasisi yake kwa kushirikiana na JAT itaanza na mafunzo kwa albino 50.
 
Brigitte alisema kuwa mafunzo hayo yanalenga sehemu kuu mbalimbali ambazo ni kujitambua (Life skills), kutathmini aina mbalimbali za biashara (Business Analysis), namna ya kutunza pesa ( How to save), kuandika mchanganuo wa biashara (Business Plan), kutembelea sehemu mbalimbali zinazoendana na biashara atakayoifanya na jinsi ya kuanza biashara.
 
Alisema kuwa BAF ikishirikiana na wadau mbalimbali na pia itagharimia gharama za mafunzo na mahitaji mbalimbali ya kuboresha hali yao.
 
“Mafunzo haya yatachukua muda wa mwaka mmoja yaani watashiriki na yataanza rasmi Agosti 18, kila mshiriki wa mafunzo haya atapatiwa kitabu chenye masomo yote ili aweze kuendelea kujisomea,” alisema Brigitte.
 
Mkurugenzi wa JAT, Maria Ngowi alisema kuwa wamejipanga kufanikisha mpango huo na wanaamini albino watakaopata mafunzo hayo watafanikiwa katika maisha yao ya kila siku.
 
Ngowi alisema kuwa JAT imejikita katika Nyanja tatu ambazo ni ujasiria mali, elimu ya kuzalisha, kuiwekeza na kutunza fedha na elimu ya kazi.
 
Alisema kuwa taasisi yao ni sehemu ya taasisi kubwa ulimwenguni inayoitwa Junior Achievement International ambayo iko katika nchi 120 duniani huku afrika ikiwa katika nchi 17.
 
Kaimu Katibu Mkuu wa Tanzania Albino Society (TAS), Mohamed Chanzi alimshukuru Brigitte na JAT kwa kuwajali na kuomba wadau mbali mbali kuwaunga mkono.
 
“Wamelenga kutusaidia kimaisha, kwani msaada wa elimu ni mkubwa kulinganisha misaada mingine, naomba wadau wawaunge mkono,” alisema Chanzi

No comments:

Post a Comment