Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
KLABU ya Simba sc inatarajia kufanya mkutano mkuu wa wanachama kesho Agosti 3 mwaka huu katika ukumbi wa Police Officers Mess Oysterbay, jijini Dar es salaam.
Mkutano huo wa kwanza kufanyika chini ya viongozi wapya wanaoongozwa na Rais Evans Elieza Aveva na makamu wake Geofrey Nyange ‘Kaburu’ utafanyika ukiwa na agenda 13 za kujadili.
Agenda inayotarajia kuwa moto wa kuotea mbali ni ile ya wanachama 72 waliosimamishwa na kamati ya utendaji akiwemo aliyekuwa mgombea wa Urais Komred, Michael Richard Wambura.
‘Kidume’ Wambura alisimamishwa uanachama wake mwaka 2010 kutokana na kosa la kuipeleka klabu mahakamani.
Wanachama wengine 69 wanakabiliwa na kosa kama hilo kwani waliipeleka klabu mahakamu kuu wakitaka kusimamishwa kwa uchaguzi mkuu uliofanyika juni 29 mwaka huu kwa madai kuwa katiba ilikiukwa.
Agenda ya kwanza katika mkutano wa kesho ni kuhakiki wanachama wanaohudhuria mkutano na agenda ya pili ni kuthibitisha Agenda za mkutano huo.
Agenda ya tatu katika mkutano huo utakaotoa hatima ya Wambura ni kuthibitisha kumbukumbu za kikao kilichopita na Agenda ya nne ni Yatokanayo na kumbukumbu ya kikao kilichopita.
Agenda ya tano ni hotuba ya Rais wa Simba, Evans Aveva na agenda ya sita ni kupokea na kujadili taarifa kutoka kamati ya utendaji.
Agenda ya saba ni kuthibitisha bajeti ya mwaka ya klabu, wakati agenda ya nane ni kuthibitisha uteuzi wa wakaguzi wa hesabu wa nje.
Agenda ya tisa ni kuthibitisha walezi na wadhamini wa klabu, wakati agenda ya kumi ni marekebisho ya katiba.
Agenda ya 11 inayotarajiwa kuwa ya vuta ni kuvute ni ile kuhusu wanachama 72 waliosimamisha na kamati ya utendaji.
Baada ya hapo, agenda ya 12 ni wanachama wa heshima na agenda ya 13 na ya mwisho ni kufunga kikao
No comments:
Post a Comment