Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
Moja ya matatizo makubwa katika soka la Tanzania ni ubinafsi, roho mbaya, kujikuza na kuwakatisha tamaa baadhi ya watu wenye nia ya kusaidia maendeleo ya soka la Tanzania. Kiongozi mwenye madaraka anatumia nafasi yake kuua ‘ madharia’ ya itikadi ambazo zinakwenda tofauti na mtazamo wake. Mambo ya soka hayaendi mahakamani, lakini inapotokea hivyo ni lazima kuwepo na sababu za msingi zinazomshawishi muhusika/wahusika kufikia uamuzi wa kwenda katika mahakama kutafuta haki ya kile wanachokuwa wakipigania kwa sababu mahakama ni sehemu ya mwisho ambayo haki upatikana.
Jumapili iliyopita klabu ya Simba SC, ilifanya mkutano wake mkuu wa wanachama na wanachama wasiozidi 600 walifikia maamuzi ya kuwafuta uanachama wenzao 72, huku pia aliyekuwa mgombea wa nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo, Michael Wambura akikutwa na ‘ kimbunga’ hicho.
Mambo mengine hayapaswi kupewa nafasi kama wadau-viongozi wa soka hawatabadilika katika itikadi zao za kiutawala. Mpira siyo tu kuwa na wachezaji wazuri, au klabu kuwa na pesa zisizo na vyanzo vya kueleweka. Mpira unahitaji ushirikiano wa watu wenye ujuzi na mambo ya kiutawala. Mtu anaweza kuwa ndani au nje ya uongozi lakini mawazo yake yanaweza kutumika kwa manufaa ya mpira wan chi. Kitendo cha kumfuta Wambura uanachama ni kufuata muongozo wa kanuni na sheria za shirikisho la soka ulimwenguni, FIFA.
Wanachama 72 waliokwenda mahakamani wakati wa uchaguzi mkuu wa klabu hiyo Mwezi, Juni pamoja na Wambura aliyeadhibiwa kwa makosa ya mwaka 2010 walikuwa katika sura tofauti. Kwa nini tena, Wambura wakati kila kitu kilikwisha pita na mtu huyo kuonekana hana hatia. Nani ambaye alimsamehe Wambura na kumuhalalilisha ‘ kuhusu usafi wake’ na mtu ambaye ana uwezo wa kuongoza Simba kutokana na kukidhi mahitaji yote ya uanachama?
Nashangaa, Evansi Aveva naye amejionyesha wazi hivi sasa kuwa hapendezwi na itikadi za Wambura, ina wezekana ilikuwa hivyo tangu mwanzo wakati kiongozi huyu alipokuwa akitupiwa makombora kuwa si mwanachama halali wa klabu wakati wa hekaheka kuelekea uchaguzi mkuu wa klabu. Wambura alitoa vielelezo vyote kuhusu uhalali wa uanachama wake na alipambana dhidi ya wale wote waliomkatia rufaa kupinga kiongozi huyo wa zamani wa Shirikisho la soka nchini kupitishwa kuwania nafasi ya urais. Kilichokuja kuonekana mwishoni ni kwamba, Wambura alikuwa mwanachama halali wa Simba huku makosa yake ya nyuma ya kuipeleka klabu hiyo mahakamani mwaka 2010 alikwisha samehewa.
Wambura hakushiriki katika uchaguzi baada ya jina lake kuondolewa wiki moja kabla ya uchaguzi mkuu kwa kosa la kufanya kampeni nje ya muda husika na kuvunja kanuni za uchaguzi. Ni kosa ambalo alifanya na hakulilalamikia hata kidogo. Wabaya wake wakafanya juu chini na kumnyima haki yake ya kikatiba ya kupiga kura siku ya uchagguzi kwa madai kwamba si mwanachama! Kivipi, mbona alikuwa na nafasi ya kusimama na kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu kama hasingefanya kampeni nje ya muda maalamu?.
Baada ya kuingia madarakani, Aveva alisema atalipeka suala la Wambura katika mkutano mkuu wa wanachama, si yeye tu aliwajumuhisha na wale wanachama wengine ambao walikwenda mahakama kuu kujaribu kuzuia uchaguzi mkuu ambao ulifanyika baada ya mahakama kutupilia mbali maombi hayo kutokana na kutokidhi vigezo. Kwa nini Aveva alimuweka Wambura katika orodha ya wanachama ambao watajadiliwa kutokana na makosa ya kwenda mahakamini wakati Wambura tayari alikuwa huru na alikidhi vigezo vyote kama mwanachama hai wakati wa uchaguzi.
Kama katiba inasema makosa ya namna hiyo yatatolewa uamuzi katika mkutano mkuu wa wanachama wote, je, ni nani ambaye alimpatia msamaha Wambura kiasi cha kuonekana ni mwanachama hai?Simba inajijenga katika mtazamo wa chuki baina yao hata katika mambo ya kawaida. Upande wangu kumfuta uanachama Wambura, haki bado haijatendeka. Maisha ya utoto yamegawanyika katika sehemu kuu nne.
Hatua ya kwanza ni utoto mchanga, huu ni wakati ambao motto huanza kujenga mazoea na tabia njema. Huu ni wakati unaofaa zaidi kumwonga motto kutawala maono yake. Kipindi cha pili, hiki ni kipindi cha kwanza cha utoto, huu ni wakati ambao motto hujifunza kutumia milango yake ya maarifa. Pia kipindi cha tatu cha ukuaji wa motto ni kipindi cha uvulana na usichana, huu ni wakati ambao motto huanza kutumia akili yake. Kipindi cha mwisho ni cha ujana, hiki ni kipindi kizuri ambacho motto anatakiwa kupewa mafunzo na elimu ya kumsaidia kukuza maadili yake, huu ni wakati ambao motto hujifunza kutofautisha kuhusu mema na mabaya, elimu ya wakati huu ni lazima iwe ile ya kumkuza motto kukua kijamii. Simba SC, ipo katika kipindi kipi cha ‘ utoto’? Kila motto huzaliwa akiwa na tabia nzuri, ila mazingira ndiyo yanayopelekea wawe na tabia mbaya, njia bora ya kuwaelimisha watoto ni kuwaweka katika hali ya usawa. Simba wanakoseana kila wakati, timu gani hii!!!
0714 08 43 08
No comments:
Post a Comment