Tuesday, August 26, 2014

DIEGO SIMEONE ASHIKISHWA ADABU NA SHIRIKISHA LA SOKA NCHINI HISPANIA, ATASUGUA BENJI MECHI NANE MFULULIZO NA ADHABU NYINGINE JUU

Shirkisho la kandanda nchini Hispania limemsimamisha meneja wa Atletical De Madrid, Diego Simeone kutokuwa kwenye benji la ufundi la timu yake katika michezo minane ijayo kwa sababau ya utovu wa nidhamu aliyo onyesha wakati timu yake ikipepetana dhidi ya mtani wake wa jadi, Real Madrid katika dimbani Vicent Calderon siku ya Ijuma ya Agosti 22 mwaka huu ambapo Atletical walishinda kwa goli 1-0.

Diego Simeone
Diego simeone ndiye kocha anaye ongoza kwa ubwatukaji katika ligi ya Hispania kwa sasa

Katika mchezo huo ambao ulikuwa ni wa kuashiria kufunguliwa kwa ligi kuu ya Hispania amabayo hufahamika kwa jina SUPER CUP, Diego Simeone alitolewa nje ndani ya dakia 24 ya mtanange huo baada ya kumfokea aliyekuwa mwamuzi wa mchezo huo, David Fernando akitaka amruhusu mchezaji wake, Juanfran Torres kurudi uwanjani haraka baada ya kumaliza kutibiwa jeraha la mdomo alilolipata baada ya kugonga na Ronaldo uwanjani.

Mchanganuo wa adahabu hiyo ni kama ifuatavyo; kwanza Simeone amesimamishwa mechi nne kwa kosa la kumgonga mwamuzi msaidizi kwenye kisogo wakati wa maabisahano, kosa la pili ni lile la kutaka kugoma kutoka nje baada ya kuamriwa kufanya hivyo kosa ambalo limemsimamisha mechi mbili , kosa la tatu ni lile la kufoka wakati akitoka nje ya uwanja ambapo kosa hili limemuweka nje mechi moja na kosa la nne ni lile la kubaki kwenye jukwaa la mashabiki badala ya kwenda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kama ambavyo sheria inasema, kosa ambalo pia limememfanya kuwa nje ya dimba mechi moja.

Mbali na kupewa adhabu ya kuwa nje ya benji la ufundi kwa jumla ya mechi nane, Diego Simeone pia ameamuriwa kulipa kiasi cha dola za kimarekani 6,339, wakati huhuo klabu yake ya Atletical yenyewe ikiamriwa kulipa kiasi cha dola za kimarekani 3,694

No comments:

Post a Comment