Tuesday, August 26, 2014

KIMENUKA BUNGE LA KATIBA--- MWANDISHI KUBENEA, AKIMBILIA MAHAKAMANI KUOKOA PESA ZA WATANZANIA SOMA HAPA KUJUA ZAIDI




Pichani niSaed Kubenea,
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited - wachapishaji wa gazeti la MwanaHALISI, lilosimamishwa na serikali kwa muda usiojulikana, MSETO, MwanaHALISI Online.com na mtandao wa MwanaHALISI Forum ambaye amefungua kesi Mahakama kuu kushinikiza Bunge Maalum la Katiba livunjwe picha na Maktaba

 Karoli Vinsent na Mwanahalisi Forum
MWANDISHI mwandamizi wa Habari nchini  Saed Kubenea ameamua kuwa Mzarendo na Nchi yake Baada ya Kufungua kesi Mahakamani kwa lengo la Kuzuia Bunge la Katiba lisiiendelee haya ndio aliyasema mwenyewe Kubenea kuhusu hilo 

“Kwa muda wa siku tatu mfululizo sasa, kumekuwa na mjadala hapa MF kuhusu mimi kufungua kesi ya kikatiba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba. Niseme wazi kwamba ni kweli nimefungua kesi hiyo; tayari kesi hiyo imepewa Na. 28/ 2014.

         Katika kesi hiyo, pamoja na mengine, nimeomba mahakama itoe tafsri sahihi juu ya mamlaka ya Bunge Maalum la Katiba, chini ya vifungu vya 25 (1) na 25 (2) vya Sheria ya Marekebisho ya Katiba namba Namba 83 ya mwaka 2011.


         Aidha, nimewasilisha maombi nikitaka mahakama itoe zuio la muda la kusimamisha bunge hilo ili kusubiri uamuzi wa maombi ya tafsiri.

          Kinyume na inavyoelezwa na kutaka kuaminishwa na baadhi ya watu, kuwa nimetumwa kufungua kesi hii; ukweli ni kwamba shauri hili nimelifungua kwa utashi wangu binafsi.

            Katika maisha yangu yote, sijawahi kutumika kwa maslahi ya mtu binafsi. Nimetumika kwa maslahi ya umma. Hivyo basi, sijasukumwa na kundi lolote kufanya kazi hii. Wala siwakilishi matakwa ya yoyote; zaidi ya maslahi ya taifa langu.

        Nimefungua kesi hii, baada ya kuona Rais wa Jamhuri, Dk. Jakaya Kikwete ambaye kwa mujibu wa katiba, amepewa mamlaka ya kusimamia rasimali za taifa, akiendelea kuruhusu mabilioni ya shilingi za walipa kodi yakitumika kwa jambo ambalo halina manufaa kwa taifa.

                 Nimefungua kesi hii, baada ya kukiona chama tawala – Chama Cha Mapinduzi – ambacho ndicho kilichopewa ridhaa na wananchi kusimamia rasimali zao, kikimuoga Samwel Sitta, mwenyekiti wa bunge hilo hivyo kumuacha akitafuna fedha za wananchi kama mchwa.

            Ninawaahidi Watanzania wenzangu, popote walipo – ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano – nitasimama katika shauri hili hadi mwisho. Sitayumba wala kuyumbishwa. Siko tayari kusikiliza yoyote zaidi ya kusimamia maslahi ya nchi yangu.

Saed Kubenea,
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited - wachapishaji wa gazeti la MwanaHALISI, lilosimamishwa na serikali kwa muda usiojulikana, MSETO, MwanaHALISI Online.com na mtandao wa MwanaHALISI Forum.



         Leo, Tarehe 25 August 2014 kwa niaba ya mteja wangu Saed Kubenea ambaye ni mwandishi wa habari mkongwe wa gazeti ya Mwanahalisi, nimefungua shauri Mahakama Kuu ya Tanzania nikiomba yafuatayo;
            1. Mahakama Kuu itoe tafsiri sahihi ya Kifungu cha 25 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.
       2. Mahakama Kuu itoe tamko iwapo Bunge Maalum la Katiba lina uwezo wa kubadili Misingi Mikuu ya Rasimu.
           3. Mahakama Kuu itoe amri ya kusimamisha Bunge Maalum la Katiba lisiendelee na vikao mpaka pale tafsiri sahihi ya Mamlaka yake itakapotolewa na Mahakama Kuu.

Kwa kuwa muda unakwenda na mabishano yanaendelea, na hakuna anayechukua hatua, nimeona ni vyema kukishirikisha chombo chenye mamlaka kamili ya Kikatiba kutoa tafsiri sahihi ya Kisheria.

Peter Kibatala, Wakili

No comments:

Post a Comment