Mohamed Hussein 'Mmachinga' (kushoto) na Edibily Jonas Lunyamila (kushoto) watakumbushia enzi zao dhidi ya Real Madrid uwanja wa Taifa
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
KIKOSI maalumu cha ‘Tanzania All Stars’ kitakachoshuka dimbani kuvaana na magwiji wa Real Madrid, ‘Real Madrid Legends’ kitaingia kambini jijini Dar es salaam kujiandaa na mechi hiyo itakayopigwa uwanja wa Taifa Agosti 23 mwaka huu.
Makocha maarufu nchini, Charles Boniface Mkwasa ‘Master’, Fredy Felix Minziro na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ wataongoza benchi la ufundi la kikosi hicho , huku Daktari wa timu akiwa ni Mwanandi Mwankemwa.
Viongozi wa timu ni Mtemi Ramadhani, Hassan Mnyenye, Omar Gumbo na Hamisi Kisiwa.
Wachezaji walioitwa kuingia kambini kwa ajili ya mechi hiyo ni makipa waliowahi kutamba nchini Tanzania, Mohamed Mwameja na Peter Manyika.
Watakaosuka safu ya ulinzi ni mabeki Shadrack John Nsajigwa Mwandemele, Boniface Pawasa, John Mwansasu, Mecky Mexime, Abubakar Kombo, George Masatu na Habib Kondo,
Viungo ni: Suleiman Abdallah Matola ‘Veron’, Shaaban Ramadhani, Salvatory Edward, Sabri Ramadhani ‘China’, Yussuf Macho Musso, Abdul Mashine, Abdul Maneno, Mao Mkami, Steven Nyenge, Akida Makunda na Mtwa Kihwelo.
Kutoka kushoto, Luis Figo, Zinedine Zidane na Ronaldo De Lima wote watakuwepo nchini Agosti 22 mwaka huu na kucheza mechi Agosti 23 uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
wWashambuliaji: Monja Liseki, Iddi Moshi, Dua Said, Emmanuel Gabriel Mwakyusa, Said Maulid ‘SMG’, Thomas Kipese, Nasor Mwinyi ‘Bwanga’, Edibilly Lunyamila, Mohamed Hussein ‘Mmachinga’, Clement Kahbuka,
Madaraka Suleiman ‘Mzee wa Kiminyio’ na Akida Makunda.
Magwiji wa Real Madrid waliotamba katika michuano ya ligi kuu nchini Hispania, La Liga, ligi ya mabingwa barani Ulaya, UEFA na kombe la dunia watatua jijini Dar es salaam Agosti 22 mwaka huu.
Mbali na kucheza mechi hiyo Agosti 23, magwiji hao waliotikisa soka la dunia watatembelea vivutio mbalimbali vya utalii nchini ikiwemo kupanda mlima Kilimanjaro.
Ziara hiyo mwaliko wa kampuni ya Tanzania Sisi na Nyumbani (TSN) chini ya mkurugenzi wake mkuu, Farough Baghozah na meneja wa ziara, Dennis Ssebo amesema maandalizi ya tukio hilo la kihistoria yanakwenda vizuri.
Ssebo alisema kiingilio cha chini katika mechi hiyo kitakuwa shilingi elfu tano tu (5,000/=).
Miongoni wa wachezaji watakokuja nchini ni Luis Madeila Figo, Zinedine Zidane, Ronaldo De Lima.
No comments:
Post a Comment