Saturday, August 30, 2014

COASTAL UNION YASHUSHA MSHAMBULIAJI MPYA KUTOKA GORMAHIA YA KENYA

         
???????????????????????????????
Mshambuliaji mpya wa Coastal Union kutoka Gormahia
ya Kenya Itubu Imbem Guelor akisaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia
timu hiyo kwenye makao makuu ya klabu hiyo barabara kumi na moja jijini
Tanga kulia ni Meneja wa timu ya Coastal Union akida Machai na kushoto ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Salim Bawaziri  jana,Picha na ,Tanga. ???????????????????????????????
kulia ni Meneja wa Klabu ya Coastal Union Akida Machai
akimuonyesha kitu kwenye simu ya mkononi, Mshambuliaji Mpya wa timu hiyo
aliyesajiliwa kutoka Gormahia ya Kenya ,Itubu Imbem Guelor aliyesaini
mkataba wa kuichezea kwa kipindi cha miaka miwili,Picha na,Tanga.
…………………………………………………………………
UONGOZI wa Coastal Union umeonyesha nia ya kusaka ubingwa wa Ligi kuu soka
Tanzania bara kwa vitendo kwa kufanya usajili wa nguvu baada ya kumpa
mkataba wa miaka miwili aliyekuwa mshambuliaji wa Gormahia ya Kenya Itubu
Imbem Guelor .
Utiliaji wa Saini hiyo ulifanyika jana makao makuu ya Klabu hiyo mbele ya
Meneja wa Coastal Union Akida Machai na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili
Salim Bawaziri
Itubu ambaye pia aliwahi kuzichezea timu za FC Leopard ya Kenya,na Tusker
amehaidi kuipa mafanikio timu hiyo ambayo imedhamiria kurudisha histori
yake ya miaka 1988 waliochukua ubingwa wa Ligi kuu Tanzania.
Mchezaji huyo anakuwa  ni wa pili kutoka timu hiyo kusajiliwa na Coastal
Union ambapo kwanza aliyesajiliwa ni Rama Salum ambaye aliingia mkataba wa
kuichezea timu hiyo hivi karibu na tayari yupo visiwani Pemba kwa ajili ya
maandalizi ya msimu mpya wa Ligi kuu .
Akizungumza kabla ya kupanda ndege kuelelekea visiwani Pemba ambapo timu ya
Coastal Union imeweka kambi kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi kuu soka
Tanzania bara,Itubu alisema amefurahishwa sana kusajiliwa na timu hiyo na
kuwahaidi wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kuwa watafanya kila
liwezekanalo kuweza kunyakua ubingwa wa ligi hiyo.
Mshambuliaji huyo ambaye ni mzaliwa wa Kongo Kinshasa alisema malengo yake
makubwa ni kuhakikisha anashirikiana na wachezaji wenzake katika kuipa
mafanikio timu hiyo.
“Kimsingi mimi mwenyewe binafsi nimefurahi sana kuja kuicheza Coastal Union
kwa sababu ni timu yenye historia kubwa ya soka hapa nchini hivyo naahaidia
kushirikiana na wachezaji wenzangu ili kutimiza ndoto walizojiweka za kuwa
mabingwa wapya Ligi kuu msimu ujao “Alisema Itubu.
Kwa upande wake, Meneja wa Coastal Union Akida Machai alisema kuwa usajili
huo ni ishara tosha ya kuwa timu hiyo itakuwa tishio kwenye michuano ya
ligi kuu Tanzania bara msimu ujao kwa kuweza kutimiza malengo yao ya muda
mrefu ya kunyakua bingwa wa Ligi kuu.

No comments:

Post a Comment