Tuesday, August 19, 2014

TISHIO LA EBOLA,WANANCHI WAKAE CHONJO


Pichani ni baadhi ya  Daktari wakiwa wamembeba mgonjwa wa EBORA picha kwa hisani ya Mtandao
————————–
Na Hannah Mayige,  wa Chuo Kikuu Huria, OUT
TISHIO la ugonjwa wa Ebola
unaoendelea kuuwa mamia ya watu Afrika Magharibi, umezua wasiwasi  mkubwa
kwa nchi za Afrika  na  dunia
nzima  kwa  ujumla na
watanzania kutakiwa  kuchukua tahadhari  kubwa kudhibiti ugonjwa huo usiingie nchini.
    Lazima  Serikali na wananchi  wazingatie masharti na tahadhari inayotolewa
kimataifa kuudhibiti ugonjwa na utayari wake wa kupambana nao.
    Ugonjwa wa Ebola, umekuwa
tishio kubwa kwa uhai na ustawi wa mataifa mbalimbali yakiwemo ya Afrika
Mashariki ambako Tanzania ni mojawapo. 
     Mpaka  sasa,
nchi  zilizoathirika  na ugonjwa
huo ni pamoja na Cameroon, Liberia na Nigeria  ambapo
tayari  zaidi  ya
watu  1,000 wamepoteza maisha.
     Eneo la Afrika
mashariki,  kuna taarifa kuwa  hivi karibuni alipatikana mgonjwa  wa Ebola
katika  nchi ya  Rwanda na kwamba miaka ya nyuma milipuko
iliwahi kutokea nchini Uganda.  
    Ebola  ni ugonjwa
ambao  mpaka  sasa hauna
tiba  wala   chanjo,
ambapo  huambukiza  kwa
njia  ya  hewa
au  majimaji  yatokayo
mwilini  kama  mate , jasho,  damu na kwamba mgonjwa  akigusana  na    mtu  asiye na
virusi  hivyo  basi  anaambukizwa.
    Shirika
la  Afya  Duniani
[WHO]  limetahadharisha  nchi
mbalimbali  hasa  Afrika
kuchukua tahadhari  kubwa, mfano  hivi
karibuni  ndege  za shirika
la  Kenya  lilishauriwa kutoendelea  na
safari  zake za  Afrika
Magharibi  kwa  kuhofia baadhi yaabiria wake  kuhamisha virusi vya Ebola na kusambaza katika
eneo la Afrika Mashariki.
      Kenya ni mojawapo
ya nchi za Afrika mashariki zenye safari nyingi za ndege kuelekea mataifa
mbalimbali.
Kutokana na wito huo wa WHO, tayari  Korea imesitisha safari zake za ndege kwenda
Kenya kwa tahadhari ya kudhibiti usambaaji wa Ebola.
     Kwa kuwa
ugonjwa  huo  unaambukiza kwa  njia
ya hewa     pia na majimaji  yatokayo mwilini  hata madaktari  na wauguzi
wanalazimika   kuwa na mavazi  maalum
ambayo yanafunika  mwili  mzima, kwani
hawatakiwi kugusana  kwa  namna
yeyote  ile.
     Msimamizi wa  Vituo vya Afya mipakani Tanzania, Dk. Khalid
Massa, anasema vifaa hivyo ni pamoja na magauni, aproni, buti, gloves na vifaa
maalum vya kuziba pua na mdomo.
      “Wahudumu
wanatakiwa kuvaa vifaa hivyo kujikinga na maambukizi na tayari vifaa 20,000
vimepokelewa na kusambazwa katika maeneo yaliyoainishwa,” anasema Dk. Massa.
Dk. Massa, anasema kwa kushirikiana na maofisa uhamiaji
wamejikita zaidi kuchunguza wasafiri wa ndege hasa wanaotokea Afrika Magharibi.
      Naye, Mtaalamu wa
Kudhibiti magonjwa ya mlipuko Dk. Vida Makundi, anawaasa wananchi kuripoti
mapema katika vituo vya afya au kwa viongozi wa serikali za mitaaa endapo
watakuwa na dalili   za ugonjwa huo.
Anazitaja dalili kubwa
ambazo  zimeelezwa  na
Shirika   la  Afya
duniani  ni pamoja  na
kuumwa   sana kichwa , kupata  homa
kali, na  hatimaye kutokwa  na damu katika  maeneo yenye
uwazi, kama vile  mdomoni, ngozi, masikioni  na sehemu za siri.
Ebola imesababisha
hofu na tafrani  kubwa  kwa nchi
hasa zinazoendelea  kwa  kuua watu bila kupata tiba ikiwa ni pamoja na
madaktari  na udhoofisha  hali
ya  uchumi  kutokana na shughuli nyingi za kusafiri na
zinazokutanisha watu kusitishwa.
Shughuli za biashara za kimataifa pia  zinaendelea kutetereka kuogopa maambukizi  ya virusi
vya Ebola hasa  wananchi katika  nchi
zenye  ugonjwa  huo
kuogopana wenyewe  kwa wenyewe.
Mfano, huko Cameroun,
kuna  mtu alikutwa amekufa  barabarani hakuna  mtu
aliyethubutu kumsogelea  mpaka
walipokuja  madaktari ambao walivalia  rasmi
kuhakikisha   hakuna maambukizi
mapya kwa watu wengine.
Hapa  Tanzania, tayari
serikali kupitia   viongozi
mbalimbali akiwemo  Makamu wa  Rais Mohamed
Ali  Bilal , Waziri wa Afya Dk.
Seif Rashid na baadhi ya wakuu wa mikoa ya Manyara, Dar es Salaam na  Mbeya  wamewataka
wananchi kuwa  waangalifu na wageni wasio
wajua   na  kuwa tahadharisha  kwenda
hospitali mara  wanapoona wana dalili  zisizo
za  kawaida  au zinazoashiria  ugonjwa
wa Ebola.
Kulingana  na tamko la
serikali ,  Ebola  bado haijaingia nchini lakini  usemi wa
Kiswahili usemao ‘ ukiona mwenzako
ananyolewa,  wewe  tia maji’.
Kwa  upande wa kutenga
maeneo maalum ya kushughulikia wagonjwa wa Ebola, serikali imetenga maeneo
mawili kwa Dare s Salaam, Temeke na Hospitali ya Taifa Muhimbili.
 Waziri wa afya  DK.  Seif
Rashid anasema tayari wauguzi na madaktari wanapatiwa elimu  kuhusiana
na kuudhibiti  ugonjwa wa  Ebola
kabla  haujaingia  nchini, elimu hiyo  inatolewa
katika  hospitali zote .
Nao, wananchi kwa nyakati tofauti wameendelea kumlilia mungu
kwa mlipuko wa magonjwa hapa barani Afrika. “Mara ukimwi, mara Dengue mara
Ebola yote hakuna tiba,” analalamika mmoja wa wananchi Kasian Komba mkazi wa
Songea. 
Kutokana na taarifa za baadhi ya wananchi wa Liberia kuvamia
kituo kilichotengwa kuhudumia wagonjwa wa Ebola na kupora magodoro, vifaa na
wagonjwa kutawanyika, ni taarifa mbaya na huenda imetokana na kukosa elimu ya
ugonjwa huo.
       Kwakuwa elimu ni
muhimu,  ni vyema serikali hapa nchini
ikatumia fursa hii kuelimisha umma kwa kutumia mikutano ya hadhara, Sanaa za
maonesho, mabango, vyombo vya habari kama mitandao ya kijamii,  redio, televisheni, magazeti na vipeperushi
ili jamii ipate uelewa.
Makala hii imeandikwa na Hannah Mayige, Mwanafunzi wa Chuo
Kikuu Huria cha Tanzania – OUT.
Anapatikana kwa E-mailhannahmayige@gmail.com

No comments:

Post a Comment