Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika sherehe za
ufunguzi wa barabara ya Mwenge- Tegeta utakaofanyika leo tarehe 1 Oktoba 2014.
Kwa mujibu wa taaria iliyotolewa na kitengo cha Mawasilano serikalini(GCU) cha Wizara ya Ujenzi,ufunguzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta wenye
urefu wa Kilomita 12.9, utafanyika kuanzia saa nne asubuhi katika eneo la
Lugalo njia panda ya Kawe.
Upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni
sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari
katika jiji la Dar es Salaam.