Sunday, September 14, 2014

Redd’s Miss Tanzania kambini, Lake Zone watia fora Dar

 

Redd’s Miss Tanzania kambiniWAREMBO 30 wenye tiketi ya kushiriki fainali ya shindano la Redd’s Miss Tanzania, jana walianza kambi huku kivutio kikubwa katika Hoteli ya JB Belmonte, ilikuwa ni kuwasili warembo wa Kanda ya Ziwa, wakiwa katika gari moja.
Warembo hao wakiwa katika gari ya Miss Lake Zone, Rachel Clavery, jana asubuhi walijumuika na wengine kuripoti katika hoteli hiyo kuanza kambi ya wiki nne kuelekea fainali ya shindano hilo litakayofanyika mwezi ujao.
Wengine walioambatana na Rachel na mikoa yao kwenye mabano, ni mshindi wa pili Mery Emmanuel (Shinyanga); mshindi wa tatu Nicoru Sarakikya (Shinyanga) na Dorrin Robert kutoka Mwanza.
Hiyo ni gari iliyotolewa na Hoteli ya Lenny Hoteli ya Geita chini ya Mkurugenzi wake Leonald Bugomola, mmoja wa wadhamini wa shindano hilo akitoa gari iliyokwenda kwa mshindi na gharama ya kambi kwa warembo 18 waliokuwa wakiwania Miss Lake Zone.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Sinza, jijini Dar es Salaam jana, mmoja wa washabiki wa burudani, John Kisute, alisema kati ya kivutio wakati wa kuwasili kwa warembo kambini, ni warembo kutoka Miss Lake Zone, kutumia gari moja la Miss Lake Zone 2014.
“Mimi ni shabiki wa urembo, nampongeza sana Mkurugenzi wa Lenny Hotel ya Geita, japo simfahamu kutoa zawadi kubwa kiasi hiki, kumeongeza hadhi na heshima ya shindano la urembo kwa ujumla,” alisema.
Akatoa wito kwa wadhamini wengine wa shindano hilo ngazi ya viyongoji hadi mkoa hadi Kanda, kutoa zawadi kubwa kuongeza hadhi, heshima na thamani ya shindano hilo ambalo limezidi kupata umaarifu mkubwa.
Akizungumza baada ya kuwasili kwa warembo hao na kupokelewa, Mratibu wa mashindano hayo, Hashim Lundega, Mkurugenzi wa Miss Tanzania, aliwapongeza kupata nafasi hiyo na kuwataka waishi kwa upendo na kuheshimiana wakati wote.
Lundenga alisema ndani ya kambi ya wiki nne, warembo hao wakiwa mjini Arusha, watapata fursa ya kutembelea vivutio kadhaa vya kitalii ikiwemo kaburi la aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine, aliyefariki mwaka 1984.
Warembo hao walionza kambi yao jana katika ukumbi wa JB Belmonte iliyoko jijini hapa huku baadhi ya wadau wa burudani wakijiuliza kama mshindi wa Lake Zone amepata gari yenye thamani ya sh mil 10, Miss Tanzania atazawadiwa nini?

chanzo Tanzania Daima

No comments:

Post a Comment